HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, October 5, 2022

Uelewa mdogo Umetajwa kuwa changamoto kwa bodaboda kuto kujiunga na mifuko ya hifadhi za kijamii

UELEWA mdogo Umetajwa kuwa ndio changamoto ya waendesha bodaboda kuto kujiunga na mifuko ya hifadhi za kijamii pamoja na bima za afya nchini.

Hayo yamesemwa na Mhadhiri wa Chuo Kikuu Mzumbe, Dkt. Godbertha Kinyondo wakati wakitoa matokeo  kwa waendesha bodaboda jijini Dar Es Salaam leo, Oktoba 5, 2022, amesema kuwa waendesha bodaboda hawana uelewa kuwa wanaweza kupata Pensheni ya Uzeeni kwani wanajua kama Pensheni inapatikana kwa Wafanyakazi wa Serikalini tuu.

Pia amewatia Moyo kuwa Kazi ya ujasiliamali mdogo mdogo na uendesha bodaboda ni kazi kama kazi nyingine hivyo waithamini na kuipenda na lazima wapate bima ya Afya ili wawe na kinga pale wanapofanya kazi zao.

Amesema Wajasiriamali wadogo na bodaboda wamewatambua kama mama lishe, Baba lishe, Wachuuzi, Machinga na watu wasiona na ofisi Maalumu.

"Sisi Chuo Kikuu Mzumbe katika Utafiti wetu tumeenda mtaani kabisa kuangalia hawa watu wanajikimu namna gani na namna ambavyo wanaweza kujikimu katika maisha yao. Mzumbe tumeazimia kwenda Mtaani, Mtaa kwa Mtaa kuamsha watu kuhusu hizi hifadhi za jamii." Amesema Dkt. Kinyondo.

Licha ya hayo ameomba jamii iweze kuwaunga mkono katika ufanyaji wa tafiti zenye tija kwa jamii kwa Ujumla.

Kwa Upande wa Mtafiti Kutoka Chuo Kikuu Mzumbe, Aloyce Gervas amesema katika utafiti wamebaini mafunzo kwa upande wa afya na usalama kwa upande wa Madereva wa bodaboda Jeshi la Polisi nchini linafanya jitihada kwa kuwapa mafunzo maderena na namna ya kujikinga na ajali zisizo Na lazima.

Amesema utafiti huo umeonesha waajiri hawawapi mikataba madereva bodabodainayowapa haki zao, wala haiwapi haki ya kupata bima za afya na kuweza kujiwekea akiba. Mikataba inaonesha kuwalinda Maslahi ya mwenye chombo badala ya Maslahi ya Dereva wa bodaboda.

Amesema eneo hilo limekuwa changamoto kwa sababu dereva bodaboda anapopata ajali akikosekana kazini siku mbili akirudi anakuta bodaboda amepewa dereva mwingine. "Jambo hilo limekuwa changamoto wa madereva wengi kwani wanakosa kipato, ajira na wanakuwa hawana uwezo wa kuendelea na maisha mwisho wa siku wanajikuta wanaingia katika Umasikini uliopitiliza." Amesem Gervas

Mwenyekiti wa bodaboda kata ya Ndugumbi, Kinondoni Dar es Salaam, Hudugu Ng'amilo amewashukuru Watafiti Chuo Kikuu Mzumbe kwa kuwapa majibu ya utafiti walio ufanya labda utatatua matatizo yanayoikabili sekta ya bodaboda.

Amesema kuw achangamoto kubwa ilikuwa ni namna ya kupata bima za afya na Mifuko ya Pensheni. hivyo basi wametupa. "Hivyo basi wametupa elimu ya namna ya kujiunga na mifuko ya kijamii na bima ya afya katika vikundi vidogo vidogo tulivyonavyo, jambo jingine ni kuto kujua kama madereva bodaboda wanaweza kupata Pensheni Uzeeni." 

Akizungumzia kuhusiana na usalama wa madereva bodaboda amesema kuwa bima za afya zitakuwa msaada mkubwa katika usalama wao pale inapotokea changamoto.

Ng'amilo ameomba elimu zaidi itolewekwa Madereva bodaboda ili waweze kuepukana na kundi la Kulaumiwa. "Siku kundi hili limeonekana ndio kundi linalovunja sheria za barabarani na kufanya Vurugu na Jamii itambue kuwa hii kazi ya udereva wa boda boda ni Ajira kama ajira zingine kwahiyo watuheshimu ili tushikamane tuendelee kufanya kazi pamoja, wanavyotutenga na kutuzarau wanatufanya tujione ni wanyonge na kuanza kufikiri kuwa hii sio kazi sawa sawa."

Kwa upande wa Dereva Bodaboda wakike, Winfrida Ligasiwa amesema mwanamke anadharauliwa na haaminiki barabarani pia wamiliki wa bodaboda nao wamekuwa wagumu kumwamini Mwanamke. Hivyo amewaomba wamiliki na abiria kuwaamini kwani wakiaminiwa na wenyewe wanajiamini zaidi.

"Mimi ninauzoefu wa miaka Minne barabarani hivyo waajiri na abiria naomba mniamini naweza kufanya kazi hii kama wanawake wengine wanaofanya kazi nyingine." Amesema Winfrida.

Ameiomba Serikali na jamii kuwaunga mkono wawnawake wanaofanya kazi ya Udereva wa bodaboda kwa sababu udereva nao ni kazi kam Kazi nyingine.
Pia Amewashukuru Watafiti kutoka Chuo Kikuu Mzumbe kwa kuwapa elimu ya kuwa na bima ya afya na kujiunga na mfuko wa Pensheni.

Kwa upande wa Ofisa operesheni kutoka chama cha wafanyakazi kwa njia ya barabara, Amani Mwinyimvua amesema lengu kubwa la kutoa elimu wa Madereva bodaboda ni kutaka kutoa uelewa kwa Madereva wote ili waweze kujiunga katika vikundi vitakavyowasaidia na kuwarahisishia kupata huduma mbalimbali hasa bima ya afya na kutetewa pale ambapo kunatokea na changamoto mbalimbali.
Mhadhiri wa Chuo Kikuu Mzumbe Ndaki ya Dar Es Salaam. Dkt. Godbertha Kinyondo akizungumza na madereva wa bodaboda wakati wa kutoa matokea ya Utafiti uliofanywa juu ya madereva bodaboda na wajasiriamali kujiunga na mifuko ya Hifadhi za jamii na boma za afya.
Kwa Upande wa Mtafiti Kutoka Chuo Kikuu Mzumbe, Aloyce Gervas akizungumza na waandishi wa habari wakti wa uwasilishaji matokeo ya utafiti wa Mifuko ya hifadhi za jamii na bima za afya.
Ofisa operesheni kutoka chama cha wafanyakazi kwa njia ya barabara, Amani Mwinyimvua akizungumza na waandishi wa habari wakati walipokutana na madereva bodaboda jijini Dar Es Salaam leo. 


Baadhi ya Madereva bodaboda wakizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo wakati Chuo kikuu Mzumbe walipowasilisha matokeo ya juu ya bima za zavya na mifuko ya kijamii kwa wadereva hao.





Matukio mbalimbali.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad