Shirika la Tanzanite Support linatoa msaada kwa makundi ya vijana kwa kuwapatia elimu na ujuzi katika fani mbalimbali.
TSO tumedhamiria kubadilisha maisha ya vijana na kuwasaidia kufikia malengo yao na kujitegemea, Kuwashawishi wao binafsi kufanya vyema, kuwa makini zaidi na nafasi zao katika nyanja zote za maisha na kazi, kwa kuwapatia taarifa, uwezeshaji, ukuzaji, ujuzi, huku ukitoa nyenzo muhimu na ushauri.
Lengo hasa ni kundi la watu ambao wako katika hali na mazingira yaliyoathiriwa hasa vijana, wanawake na watoto. Kwa vijana juhudi zetu ni kwa wale walio katika nyumba za kulea watoto na ambao hawawezi tena kuhudumiwa katika vituo hivi baada ya kufikia umri wa miaka 18. Lengo ni kuwawezesha kujisimamia wenyewe baada ya kuondoka kwenye vituo vyao. Tunafanya hivi kupitia elimu na uwezeshaji wa kiuchumi. Tunawaingiza katika programu yetu ya “Achieving Self-Reliance” (ASR) ambayo inawatayarisha kutekeleza malengo yao. Tunafanya kazi haswa na vijana wenye umri wa miaka 15-18 kwa mpango huu.
Tunafanya kazi na wadau mbalimbali katika hatua zote za programu zetu. Vituo vya kulea watoto na mashirika mengine ambayo yanaweza kufikia vijana wanaoishi katika mazingira magumu. Tunawaleta katika kituo chetu na kuwapatia mafunzo, na kozi za kujiandaa kwa maisha ikijumuisha afya ya akili.
Katika kila hatua tunafanya kazi na washirika ambao aidha, hutoa huduma kama vile mafunzo ya kujitolea, mpango wa stadi za maisha na matokeo yake ni kuwapatia mafunzo ya kazi na ajira ambayo TSO inafuatilia ili kuhakikisha walengwa wanaishi maisha yenye mafanikio na kutimiza malengo yao.
Tembelea www.https://tanzanitesupport.org
No comments:
Post a Comment