KATIKA kuadhimisha wiki ya huduma kwa wateja Benki ya NMB Tawi la Mirerani Wilayani Simanjiro Mkoani Manyara, imesherehekea wiki hiyo pamoja na wateja wake.
Meneja wa huduma kwa wateja wa Benki ya NMB Tawi la Mirerani Bahati Philemon akizungumza na wateja wake katika kuadhimisha wiki ya huduma kwa wateja anasema kauli mbiu yao ni 'huduma kwetu ni shangwe'.
Bahati amewaeleza wateja wa benki hiyo waliohudhuria tafrija hiyo kuwa wamejipanga kikamilifu kuhakikisha wanaendelea kutoa huduma bora zaidi.
"Katika mwezi huu wa 10 kwenye maadhimisho ya wiki ya huduma kwa wateja tutafanikisha kwa vitendo kauli mbiu hii ya huduma kwetu ni shangwe,'' amesema Bahati.
Hata hivyo, katika kuadhimisha wiki hiyo ya huduma kwa wateja, Meneja wa NMB Tawi la Mirerani Alan Kombe na wafanyakazi wa benki hiyo walifanya usafi na kukabidhi makasha ya kuhifadhia taka kwenye soko la getini.
Afisa mtendaji mkuu wa mamlaka ya mji mdogo wa Mirerani (TEO) Evence Mbogo ameishukuru benki ya NMB kwa kuwapatia vifaa hivyo vya kusafisha taka.
"Pamoja na kuishukuru NMB bado tunaomba benki hiyo ituongezee vifaa vingine kwani soko letu ni kubwa na pia wanaotumia soko letu tunzeni haya makasha mliyooatiwa na NMB," amesema Mbogo.
No comments:
Post a Comment