HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, October 17, 2022

MSD: MPANGO WA DRONE KUSAMBAZA DAWA 'UMEPATA KIFAFA'+video

 

Mkurugenzi Mkuu wa Bohari ya Dawa (MSD), Mavere Tukai amesema kuwa mpango wa kusambaza dawa kwa kutumia ndege isiyo na rubani aina ya Drone si kipaumbele chao kikubwa, bali kipaumbele ni kuhakikisha dawa zinapatikana kwa wingi nchini.

Tukai amebainisha hilo alipokuwa akizungumza na vyombo vya habari katika Ukumbi wa Idara ya Habari -MAELEZO jijini Dodoma Oktoba 17, 2022, kuhusu utekelezaji wa majukumu ya bohari hiyo.

Mkurugenzi wa Idara ya Habari-MAELEZO, Gerson Msigwa akihitimisha mkutano huo kwa kutoa pongezi kwa Mkurugenzi Mkuu wa MSD,Tukai kwa kueleza na kufafanua vizuri majukumu ya bohari hiyo.


Mdau, nakuomba uendelee kusikiliza kupitia clip hii ya video, Mkurugenzi Mkuu wa MSD, Tukai pamoja na mambo mengine akielezea kuhusu mpango huo wa Drone kupata kifafa.... IMEANDALIWA NA RICHARD MWAIKENDA
MSIMAMIZI MKUU
KAMANDA WA MATUKIO ONLINE TV
0754264203

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad