HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, October 4, 2022

MAMLAKA ZA SERIKALI ZA MITAA WAPENI FURSA KATIKA VIKAO VYA MAAMUZI: MAJALIWA

 

Na WMJJWM, Dodoma
WAZIRI Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa ameziagiza mamlaka za Serikali za Mitaa kuwashirikisha Wazee kupitia mabaraza yao kushiriki kwenye vikao vya maamuzi kuanzia ngazi za vijiji na mitaa hadi Mabaraza ya Madiwani.

Akizungumza kwa niaba ya Mhe. Majaliwa, Waziri wa Nchi Ofisi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge na Uratibu Mhe. George Simbachawene wakati wa maadhimisho ya Kitaifa ya Siku ya Wazee yaliyofanyika Jijini Dodoma Oktoba 03, 2022.

Mhe. Majaliwa amesema Serikali inafanya jitihada mbalimbali kwa lengo la kuhakikisha Jamii inawatambua na kuwathamini wazee ikiwemo kuanzisha Kampeni ya mpishe Mzee kwenye maeneo mbalimbali ya kutolea Huduma.

"Kila Halmashauri iweke maeneo mazuri ya kukaa wakati wa mikutano ya mabaraza ya Madiwani na Wazee wanapo jadili mambo yao mzingatie Uzalendo na ujenzi wa maadili mema kwa watoto wetu" amesema Simbachawene

Simbachawene amemshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa kutambua Makundi muhimu hususani Wazee kwa kuanzisha Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum kwa ajili ya kushughulikia Makundi hayo kwani kabla

Makundi hayo yalikuwa ,yanakosa mahali maalum pa kupeleka Masuala yao .
Ameongeza kwamba, Serikali inaendelea kuelimisha jamii kuzingatia ulinzi na usalama kwa Wazee Kwa kuanzisha mabaraza ya wazee 20749 Kwa lengo la kuwapa fursa ya kujadili mambo yao na kuwa chombo cha kushauri Jamii.

Waziri Simbachawene ametumia nafasi hiyo kutoa Rai kwa viongozi na Wazee kuwa pamoja na kutumia mabaraza hayo kujadili Ustawi wao wahakikisha umoja na Jumuiya nyingine za Wazee zinatambuliwa na kusajiliwa katika maeneo yao na taarifa za utekelezaji wa mabaraza ya Wazee zijumuishwe kwenye kamati za Maendeleo ili mawazo yao yaweze kuzingatiwa na kufanyiwa kazi.

Ametoa wito kwa Jamii kushirikiana kuzuia ukatili kuliko kunyamaza na hatimaye kunung'unuka na kuombolea matukio yanapotokea.

Kwa upande wake Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Mhe. Dkt. Dorothy Gwajima amesema maadhimisho hayo ni matokeo ya maamuzi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan kuanzisha Wizara hii.

"Uzinduzi wa Baraza la Taifa la Wazee ni ishara ya Serikali kuwathamini Wazee kupitia mabaraza yao

Akizungumza katika Maadhimisho hayo Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais TAMISEMI Dkt. Grace Magembe amebainisha kuwa, TAMISEMI imeendelea na zoezi la kuwatambua wazee na hadi sasa imetambua 2117637 kutoka Mikoa yote 26 bapo wanaume ni 1382468 na wanawake 735169.

"Tumetoa Bima ya Afya ya Jamii kwa Wazee ili wapate huduma kwenye vituo vya Afya ngazi ya msingi kuanzia zahanati Hadi hospitali za Wilaya" amesema Dkt. Grace.

Dkt. Grace ameongeza kuwa, katika kukabiliana na changamoto ya Maafisa Ustawi wa Jamii, kibali limetolewa cha kuajiri Maafisa hao 65 ambao wamepangwa kwenye vituo vya kutolea huduma za afya ili wakatekeleze sera ya Mzee kwanza.

Naye Mwenyekiti wa Kamati ya Huduma na Maendeleo ya Jamii, Mhe Stanslaus Nyongo amesema wabunge wapo tayari kuhakikisha mchakato wa kupitia sera ya Wazee na kutungiwa sheria ya Wazee unakamilika.

Akizungumza kwa niaba ya Wazee, Mwenyekiti wa Baraza la Wazee Taifa Mzee Lameck Sendo ametumia nafasi hiyo kumpongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan Kwa juhudi kubwa anayoifanya ikiwemo miradi mikubwa, kuhamasisha Utalii ambapo mingi imeongeza ajira kwa vijana.

Amesema Wazee wapo pamoja na Mhe Rais. katika ujenzi wa Taifa ambapo
tangu kuzinduliwa kwa baraza la Wazee ambao mchakato wake ulianza 1998 baada ya utafiti kubainisha Wazee walikuwa na changamoto ya ukatili, kutengwa na familia, kuachiwa mzigo wa Malezi ya watoto hawakuwa na pa kusemea.

"Jumla ya mabaraza 20749 yameundwa tunaendelea kuimarisha Mawasiliano Kwa mabaraza yote na kupata taarifa kwa muda mfupi" amesema Mzee Sendo.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad