MAKAMU WA KWANZA WA RAIS ATEMBELEA WAGONJWA SURUA HOSPITALI YA MNAZI MMOJA - MTAA KWA MTAA BLOG

HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, October 28, 2022

MAKAMU WA KWANZA WA RAIS ATEMBELEA WAGONJWA SURUA HOSPITALI YA MNAZI MMOJA


MAKAMU wa Kwanza wa rais wa Zanzibar Mhe. Othman Masoud Othmani, ameutaka Uongozi wa Wiazara ya Afya Zanzibar kufanya jitihada ya kuelimisha na kujenga uwelewa kwa  jamii kuhusu mripoku kuwepo mripuko wa ugonjwa Surua.

Mhe. Othman ameyasema hayo huko katika hopsitali ya Rufaa  Mnazi mmoja Baada ya kuwatembelea watato wanaougua surua waliolazwa katika hospitali hiyo kuendelea na matibu na kuona hali halisi kuhusu tatizo hilo livyo hapa Zanzibar .

Mhe. Makamu ameeleza kwamba kufanya hivyo ni silaha  mihimu inayoweza kuongeza nguvu kwa jamii na serikali kwa pamoja kuweza kukabiliana vyema na ugonjwa huo na hatimae kuudhibiti na kumalizima katika kipindi kifupi.

Amefahamisha kwamba kufanya hivyo kutaondosha kuwepo mkanganyiko na upotoshaji wa taarifa unaofanywa na baadhi ya watu kulielezea suala hilo kinyume na hali hali na kusababisha sintofahamu kwa wananchi n ahata wageni wanaopanga kuitembelea Zanzibar.

Mhe. Othman amesema kwamba tatizo la surua lililojitokeza katika kipindi  cha miezi michache iliyopita Zanzibar sio la wizara ya Afya ama serikali  bali linawahusu wazanzibari wote na kila mmoja anapaswa kushiriki katika mapambano hayo ili kuumaliza kabisa ugonjwa huo.

Hata hivyo, Mhe. Othman amesema kwamba namna linavyoelezwa na tatizo hilo nje ya jamii ya wazanzibari ni kinyume na hali halisi na kuwataka wataalamu wa wizara ya afya kuhakikisha wanawaeleza wananchi na jamii kwa jumla kuhusu hali halisi ya suala hilo hapa Zanzibar

Amesema kwamba suala la mripuko wa maradhi hayo ni lazima lichukuliwe kama ni tatizo la kitaifa kwa kuwa athari inayopatikana inamgusa kila mmoja na kwamba ushiriki wa kila taasisi yakiwemo Mashirika ya kimataifa.

Amefahamisha kwamba wananchi wanapaswa kuunga mkono juhud na mipango mbali mbali  serikali katika kukabaliana na kupambana na tatizo hilo ili kuweza kuudhibiti na kuondosha kabisa usiendelee kuathiri zaidi watoto.

Mapema Mkugrugenzi wa Kinga na Elimu ya Afya Zanzibar Dk. Salimu Nassir Slimu amsesma kwamba maradhi hayo yalianzia katika wilaya ya Magharibi A na B unguja na kwamba licha ya kufanywa chanjo katika wilaya hizo lakini yaliweza kusambaa katika wilaya nyengine za Zanzibar.

Amesema kwamba toka kutoka kwa ugonjwa huo tayari zaidi ya wagonjwa 1315 na kesi 997 unguja na Pemba 318 Pemba na jumla ya watoto wannane wamefariki.

 Amefahamisha kwamba wengi waowalioathirika ni  ni watoto chini ya umri wa miaka mitano ambapo waathirika zaidi ni watoto wenye lishe duni ambao afya zao ziko dhaifu kuhimili vishindo vya maradhi mbali mbali.

Amesema kwamba hali ya kutoka kwa maradhi ni matokeo ya kutokuwepo chanjo kamilifu kwa watotoi wengi na kwamba watoto waliochanjwa kwa ukamilifu hata akiweza kupata maradhi ya surua hawezi kupata athari kubwa ikilinganishwa na asiyecvhanjwa.

Amefahamisha kwamba katiuka kukabiliana na tatizo hilo ifikapo tarehe 10 Disemba mwaka huu wa 2022, wizara hiyo inakusudia kuwachanja watoto wote waliopo Zanzibar ili kuhakikisha kwamba suala hilo linadhibitiwa katika maeneo yote ya Zanzibar.

Naye Daktari Bingwa wa watoto ambaye pia ni mdhamini wa Wodi ya maradhi hayo Dk. Zubeida Mohammed Hussein amesema kwamba karibu wagonjwa 300 wa maradhi hayo ambao wengi wao ni watoto wanapokelewa kila mwezi katika hospitakli hiyo hivi sasa.

Hata hivyo Dk. Zubeda amesema kwamba changamoto kubwa iliyopo katika kupambana na maradhi hayo ni pamoja na uhaba wa vuitendea kazi pamoja na ufinyu wa nafasi kutokana na ongezeko la wagonjwa hao ambapo baadhi wanalala kitanda kimoja wagonjwa wawili.

Mkamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Othman Masoud Othman (kushoto), akipokea maelezo kuhusu wagonjwa wa Surua  kutoka kwa Daktari Bingwa wa Magonjwa ya watoto Dokta Zubeida Mohammed Hussein(kulia) wakati Mhe. Othman alipotembelea wodi waliolazwa wagonjwa wa surua katika hospitali ya Rufaa ya Mnazi mmoja mjini Zabzibar leo tarehe 28.10.2022.  ( Picha na Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Kitengo cha Habari)
Mkamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Othman Masoud Othman (kushoto), akipokea maelezo kuhusu wagonjwa wa Surua  kutoka kwa Daktari Bingwa wa Magonjwa ya watoto Dokta Zubeida Mohammed Hussein(kulia) wakati Mhe. Othman alipotembelea wodi waliolazwa wagonjwa wa surua katika hospitali ya Rufaa ya Mnazi mmoja mjini Zabzibar leo tarehe 28.10.2022.  ( Picha na Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Kitengo cha Habari).
Mkamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Othman Masoud Othman (kulia), akipokea maelezo kuhusu wagonjwa wa Surua huko katika Ofisi za Wizara ya Afya kutoka kwa Mkurugenzi wa Kinga na Elimu ya Afya Zanzibar Dk. Salim Nassor Slim (kulia) baada ya Mhe. Othman kutembelea wodi waliolazwa wagonjwa wa surua katika hospitali ya Rufaa ya Mnazi mmoja mjini Zabzibar leo tarehe 28.10.2022.  ( Picha na Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Kitengo cha Habari.

Mkamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Othman Masoud Othman , akizungumza na watendaji wakuu wa wizara ya Afya Zanzibar katika Ofisi za Wizara hio Mnazi moja mjini Zanzibar baada ya Mhe. Othman kumaliza ziara fupi ya kutembelea wagonjwa wa Surua katika hospitali ya Rufaa ya Mnazi mmoja mjini Zabzibar leo tarehe 28.10.2022.  ( Picha na Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Kitengo cha Habari).


No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad