HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, October 28, 2022

Madiwani waomba serikalia ipige marufuku michezo ya kubahatisha

 


Madiwani wa halmashauri ya wilaya ya Njombe wameomba serikali ilidhie kuondolewa kwa michezo ya kichina ya kubahatisha (Gulugulu) kwenye maeneo yao vijijini kwa kuwa yanatajwa kusababisha vibaka huku pia watoto wa shule za msingi wakiacha shule na kuingia kwenye michezo hiyo kinyume na sheria.

Wamebainisha hayo katika kikao cha baraza la madiwani cha kujadili taarifa za kata na kubainisha kuwa wamekuwa na hofu kubwa ya wezi na vibaka ambao huenda wametokana na michezo hiyo kwasababu wimbi la vijana wanashindwa kufanya kazi wakishinda siku nzima wakijihusisha na michezo hiyo ya kubahatisha.

“Kama kuna uwezekano yaondolewe kwasababu wananchi wanalalamika Sana kutolana na vibaka na wezi na sisi tunahisi hawa wanatafuta hela ili asubuhi aende kucheza hayo magulugulu”Amesema Neema Mbanga diwani wa viti maalum

Kalokora Almachius ni kaimu mkuu wa idara ya viwanda,biashara na uwekezaji wa halmashauri hiyo amesema michezo hiyo inaendeshwa kwa mujibu wa sheria ya fedha 2019- 2020 lakini serikali imeweka utaratibu wa kuendesha ikiwemo watendaji wa vijiji na kata kuhakikisha biashara hiyo inafunguliwa kuanzia saa nane mchana na kufungwa saa nne usiku ili asubuhi wananchi wapate muda wa kuzalisha,kutoruhusiwa kwa watoto sente muri chini ya miaka 18 huku pia muendeshaji akitakiwa kuwa na deseni ya biashara.




No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad