MAADHIMISHO YA MIAKA 50 YA NBAA YAPAMBA MOTO - MTAA KWA MTAA BLOG

HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, October 20, 2022

MAADHIMISHO YA MIAKA 50 YA NBAA YAPAMBA MOTO

 Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu Tanzania(NBAA) inataraji kufanya maadhimisho ya miaka 50 tangu uanzishwa kwa bodi hiyo mwaka 1972 ambayo ilianzishwa kwa Sheria ya Wahasibu na Wakaguzi  wa Hesabu iliyofanyiwa marekebisho mwaka 2021.

Akizungumza na waandishi wa habari Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu (​NBAA), CPA Pius A. Maneno amesema Bodi hiyo imeazimia kufanya shughuli mbalimbali kwa wadau wake akiwa ni sehemu ya kuadhimisha miaka 50 ya Bodi hiyo.

Maneno amesema kuwa kuanzia Novemba 10 Hadi 12 mwaka 2022 NBAA imeazimia kufanya Clinic katika viwanja vya mnazi mmoja ili kuwaelimisha Wafanyabiashara na wananchi wote kwa ujumla jinsi ya kuandaa taarifa za hesabu za Fedha, Kodi na kuwasaidia kwenye nyanja mbalimbali zinazohusu Uhasibu na ukaguzi.

Amaesema kwenye clinic hiyo NBAA itaungana na wadau wake mbalimbali kama vile makampuni ya Uhasibu na ukaguzi, Mamlaka ya Mapato, Mamlaka ya Bima, vyuo vikuu na vyuo vinavyofundisha Masomo ya Uhasibu pamoja na mabenki katika kutoa Huduma mbalimbali ikiwa ni pamoja na kishiriki kwenye maonyesho hayo bure.

"Kutakuwa na Mashindano ya hesabu Bora zilizokaguliwa na kupata hati safi kwa mwaka 2021 na washinfi watakabidhiwa  zawadi zao tarehe 30 mwezi Novemba mwaka 2022 ambapo ni kilele cha maadhimisho ya Miaka 50 ya Bodi hiyo." alisema Maneno

Pia amesema tarehe 10 Novemba ni siku ya wahasibu duniani hivyo kama sehemu ya maadhimisho ya Miaka 50 ya Bodi hiyo NBAA kwa kushirikiana na Chama cha wanawake Wahasibu, Chama cha Wahasibu na Taasisi ya ukaguzi wa ndani wataandaa chakula  cha jioni katika hotel ya Rotana jijini Dar es Salaam.

"Tarehe 12 Novemba 2022 kutakuwa na matembezi ya hisani yatakayoanzia katika viwanja vya mnazi mmoja yakiwa na lengo la kuchangisha vitabu vya kufundishia Masomo ya Uhasibu katika shule za Serikali ambapo mgeni rasmi wa matembezi hayo atakuwa ni Waziri wa Elimu na mafunzo." alisema Maneno

Pia amesema kutakuwa na mshindano ya mpira wa miguu kuanzia tarehe 13 Hadi 28 Novemba katika viwanja vya TPDC Mikocheni. Pia amesema shughuli hizo za maadhimisho zitajitimishwa Novemba 30 mwaka 2022 katika Kituo cha mikutano cha APC Bunju jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu (​NBAA), CPA Pius A. Maneno akizungumza na waandishi wa habari kuhusu maadhimisho ya Miaka 50 ya Bodi hiyo kwenye ukumbi wa APC Bunju jijini Dar es Salaam.No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad