HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, October 17, 2022

‘HEET’ YAANZA KWA KUWAJENGEA UWEZO WANATAALUMA WA MZUMBE

 Wanataaluma wa Chuo Kikuu Mzumbe wameanza kupatiwa mafunzo ya kuboresha na kuandaa

mitaala mipya kupitia mradi wa Mageuzi ya Elimu ya Juu Kiuchumi ‘HEET’ ulioanza
kutekelezwa na chuo hicho hivi karibuni, baada ya fedha za mradi kutolewa na Benki ya Dunia
kupitia Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia.

Akizungumza katika warsha iliyofanyika Kampasi Kuu Morogoro, Mratibu wa mafunzo ya
mitaala kupitia mradi wa ‘HEET’ Dkt. Joseph Sungau, amesema warsha hiyo imelenga
kuwawezesha wanataaluma kuhuisha na kuandaa mitaala mipya kwa kuzingatia miongozo
iliyopitishwa itakayowezesha kuandakiwa Program mpya zinazoendana na soko la ajira pamoja
na kuongeza udahili wa Wanafunzi, ambalo ndiyo lengo kuu la mradi wa “HEET”.

“Tunategemea ndani ya miaka mitatu ya utekelezaji wa mradi huu, mitaala 15 ya Chuo Kikuu
Mzumbe itakuwa imeboreshwa na mipya kuanzishwa, na katika miaka mitano ya mradi
tutakuwa tumepata wahitimu watakaokuwa wanakidhi mahitaji ya soko la ajira, kutokana na
mitaala mipya iliyoboreshwa” alisisitiza Dkt.Sungau.

Katika hatua nyingine Mwezeshaji wa mafunzo hayo ambaye pia ni Mhadhiri Mwandamizi wa
Uchumi wa Chuo Kikuu Mzumbe, Dkt.Jenipher Sesabo, amesema kuwa mafunzo hayo ni
muhimu kwani yatapelekea mabadiliko chanya ya kiuchumi, hususani katika kipindi hiki
ambacho Taifa limejielekeza katika kuimarisha uzalishaji wa viwanda.
 Amesisitiza wahitimu
wanatakiwa kuwa na ujuzi na uwezo wa kujiajiri na kuajiri wengine, badala ya dhana ya sasa
iliyojengeka miongoni mwa wengi ya kuajiriwa
Kwa upande wao wanufaika wa mafunzo hayo wamesema yatawasaidia kutengeneza mitaala
inayohitajika sokoni kwani wengi wao hawakuwa na uelewa kuhusu mchakato mzima wa
kufanya maboresho ya mitaala na kuanzisha mitaala mipya, ikiwemo kufanya uchambuzi
yakinifu wa mahitaji ya soko pamoja na kujifanyia tathmini binafsi.

“Mafunzo haya ni muhimu sana kwani leo tumeweza kujua umuhimu wa kufanya tathimini ili
kutambua ikiwa tunachowalisha wanafunzi wetu ndicho kinachohitajika sokoni. Ni vema
wanataaluma wengi zaidi wakapata mafunzo haya yatakayowawezesha kutengeneza program
zinazokidhi mahita ya soko”. Alisema Dkt. Nicholous Tutuba Mhadhiri Mwandamizi wa Shule.
ya Biashara ya Chuo Kikuu Mzumbe.
Mwezeshaji wa mafunzo, Mhadhiri Mwandamizi wa Uchumi, Chuo Kikuu Mzumbe Dkt.
Jenipher Sesabo, akitoa mafunzo kwa washiriki.
Baadhi ya Washiriki wa mafunzo wakimsikiliza kwa makini mwezeshaji wa mafunzo
(hayupo pichani).
Mhadhiri wa Chuo Kikuu Mzumbe, Bw. Anosisye Kesale, akichangia mjadala wa
uboreshaji mitaala wakati wa mafunzo.
Washiriki wakifuatilia kwa makini uwasilishaji wa mada wakati wa mafunzo.
Mhadhiri wa Chuo Kikuu Mzumbe, Dkt. Patrick Kihoza, akichangia mada wakati wa
mafunzo.Dkt.Nicholous Tutuba, Mnufaika wa mafunzo akichangia mada wakati wa mafunzo.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad