Meneja
Masoko wa Halotel, Sakina Makabu (Kulia) pamoja na Meneja Mahusiano na
Stella Pius ( kwanza Kushoto), Mkuu wa shule ya Sekondari Bangulo ( Pili
kulia), Diwani wa kata ya Pugu Station Mh; Shabani Musa ( katikati) na
Mwenyekiti wa Serikal ya Mtaa wa Bangulo ( Pili Kushoto) kwa pamoja
wakibeba moja kati ya Samani zilizotolewa kwa Shule ya Sekondari ya
Bangulo Dar es Salaam wakati wa tukio la kukabidhi Vifaa hivyo leo kama
moja ya msaada na muendelezo wa mkakati wa kuisaidia sekta ya Elimu
ikiwa Kampuni hiyo ikiendelea kuadhimisha miaka Saba ya kutoa Huduma za
Mawasiliano hapa nchini.
Meneja
Masoko wa Halotel Sakina Makabu akiongea na waandishi wa habari leo
katika shule ya Sekondari Bangulo iliyoko wilaya ya Ilala jijini Dar es
Salaam leo katika tukio la kukabidhia vifaa mbali mbali vya shule
kwaajili ya kuboresha mazingira ya Waalimu ofisini na kuongeza ufanisi
wa walimu kufundisha na wanafunzi kujifunza ikiwa ni moja ya msaada
kutoka kampuni ya simu ya Halotel katika kuendana na kuadhishimisha
Miaka saba (07) ya Kampuni hiyo kutoa huduma za Mawasiliano hapa nchini.Mkuu
wa Shule ya Sekondari Bangulo Bw. Hussein Ramadhani Mwamtuya akiongea
na waandishi wa habari leo katika shule ya Sekondari Bangulo iliyoko
wilaya ya Ilala jijini Dar es Salaam leo katika tukio la kukabidhia
vifaa mbali mbali vya shule kwaajili ya kuboresha mazingira ya Waalimu
ofisini na kuongeza ufanisi wa walimu kufundisha na wanafunzi kujifunza
ikiwa ni moja ya msaada kutoka kampuni ya simu ya Halotel katika
kuendana na kuadhishimisha Miaka saba(07) ya Kampuni hiyo kutoa huduma
za Mawasiliano hapa nchini.
Diwani
wa Kata ya Pugu Station Bw; Shabani Musa akiongea na waandishi wa
habari leo katika shule ya Sekondari Bangulo iliyoko wilaya ya Ilala
jijini Dar es Salaam katika tukio la kukabidhia vifaa mbali mbali vya
shule kwaajili ya kuboresha mazingira ya Waalimu ofisini na kuongeza
ufanisi wa walimu kufundisha na wanafunzi kujifunza ikiwa ni moja ya
msaada kutoka kampuni ya simu ya Halotel katika kuendana na
kuadhishimisha Miaka saba(07) ya Kampuni hiyo kutoa huduma za
Mawasiliano hapa nchini.
Afisa
Elimu wa Sekondari wilaya ya Ilala Bw; Gerald Kwingwa akiongea na
waandishi wa habari leo katika shule ya Sekondari Bangulo iliyoko wilaya
ya Ilala jijini Dar es Salaam katika tukio la kukabidhia vifaa mbali
mbali vya shule kwaajili ya kuboresha mazingira ya Waalimu ofisini na
kuongeza ufanisi wa walimu kufundisha na wanafunzi kujifunza ikiwa ni
moja ya msaada kutoka kampuni ya simu ya Halotel katika kuendana na
kuadhishimisha Miaka saba(07) ya Kampuni hiyo kutoa huduma za
Mawasiliano hapa nchini.
Mwenyekiti
wa Serikali ya Mtaa Bangulo Bw. Goodluck Mwele akiongea na waandishi wa
habari leo katika shule ya Sekondari Bangulo iliyoko wilaya ya Ilala
jijini Dar es Salaam katika tukio la kukabidhia vifaa mbali mbali vya
shule kwaajili ya kuboresha mazingira ya Waalimu ofisini na kuongeza
ufanisi wa walimu kufundisha na wanafunzi kujifunza ikiwa ni moja ya
msaada kutoka kampuni ya simu ya Halotel katika kuendana na
kuadhishimisha Miaka saba(07) ya Kampuni hiyo kutoa huduma za
Mawasiliano hapa nchini.
**************************
Dar es
Salaam,Oktoba 20, 2022 Kampuni ya simu za mkononi ya Halotel hapa
nchini imetoa msaada wa vifaa mbalimbali vya masomo kwa waalimu na
wanafunzi wa shule ya sekondari Bangulo ili kupunguza changamoto za
mahitaji ya vifaa vya elimu zinazowakabili.
Akitoa taarifa hiyo
leo wakati wa kukabidhi vifaa hivyo katika shule hiyo Jijini Dar es
salaam, Mkuu wa Kitengo cha Bidhaa na Mawasiliano wa Kampuni hiyo,
Sakina Makabu, amesema wameamua kusaidia vifaa hivyo kutokana na
changamoto zinazozikabili shule hiyo.
Aidha, Sakina amesema
mpango huo ni kuunga mkono juhudi za serikali ambazo zimekuwa katika
kuhakikisha shule zote nchini zinapata mahitaji na vifaa muhimu
vitakavyowezesha wanafunzi kupata elimu katika mazingira bora ili kukuza
kiwango cha ufaulu wa wanafunzi hao na katika kupunguza uhaba wa vifaa
vya elimu kwa shule zote nchini.
“Halotel tumeamua kutoa msaada
huu wa vifaa ambavyo ni meza na viti vya waalimu, kabati la vitabu na
mafile, desktop mbili na printer ikiwa ni mojawapo ya muitikio wa
kampuni yetu wa kuitikia juhudi za serikali katika uboreshaji wa
mazingira na upatikanaji wa vifaa vya ufundishaji na kujifunzia ili
kuongeza ufanisi wa kufundishia na kujifunzia katika mfumo wa nadharia
na vitendo”. Aliongeza Sakina.
Pamoja na hilo, Halotel inatoa
huduma ya kimasomo ijulikanayo kama ‘Halostudy” hili ni huduma ya
kujisomea mtandaoni inayowawezesha wanafunzi kusoma mitaala ya masomo
mbalimbali nchini kwa njia ya mtandao (TEHAMA) inayopatikana kwenye simu
za mkononi na kwenye kompyuta ambapo wanafunzi na walimu kote nchini
wanatumia bure,hivyo kupitia kompyuta tulizotoa leo Shule ya Sekondari
Bangulo itaweza kutumia huduma hii kwenye kompyuta hizi.
Vile
vile hatujaishia kwa shule za sekondari tu, kwa sasa tuna mpango mpya wa
kuboresha zaidi sekta hii kidigitali kwa ngazi ya wanafunzi wa vyuo
vikuu vyote hapa nchini. Huduma hii itawawezesha wanafunzi wote vya vyuo
vikuu hapa nchini kuweza kuwekewa vocha yenye thamani ya Tsh 1,500 kila
mwezi.
Kwa upande wake Mkuu wa shule ya sekondari Bangulo Bw.
Hussein Ramadhani Mwamtuya alisema, “ Tumefarijika sana kwa kupokea
msaada huu kutoka Kampuni ya simu ya Halotel, tunawashukuru sana kwa
kuendelea kuwa karibu na jamii na kuthamini lakini pia kwa kuunga mkono
jitihada za kuisaidia sekta ya elimu nchini. Ninaamini kabisa vifaa hivi
vitawasaidia walimu na wanafunzi hapa shuleni katika kuboresha namna ya
ufusnishaji na kujifunza kwa ujumla”.
Halotel itandelea
kushirikiana na serikali pamoja na wadau wengine wa elimu katika
kuhakikisha na kufanikisha kusonga mbele sekta ya elimu ikiwa ni pamoja
na kutengeneza wanafunzi bora wanaosoma masomo ya sayansi hasa kuelekea
ukuaji wa uchumi wa viwanda.
Thursday, October 20, 2022

HALOTEL YATOA MSAADA WA VIFAA VYA MASOMO KWA SHULE YA SEKONDARI DAR ES SAALAM.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment