DC MBONEKO AWATAKA WANANCHI NA TAASISI MKOANI SHINYANGA KUTUMIA MAFUNDI UMEME WENYE LESENI ZA EWURA - MTAA KWA MTAA BLOG

HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, October 12, 2022

DC MBONEKO AWATAKA WANANCHI NA TAASISI MKOANI SHINYANGA KUTUMIA MAFUNDI UMEME WENYE LESENI ZA EWURA

 

Picha ya pamoja Mgeni  Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko  na wafanyakazi wa EWURA mara baada ya kufunguliwa kwa  semina

Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Bi.Jasinta Mboneko (kushoto) akimkabidhi Bwana Charles Jackson (kulia) ambaye ni fundi umeme, leseni ya daraja C ya ufungaji umeme ambayo imetolewa na EWURA.
Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Jansita Mboneko akifungua semina ya mafundi umeme kanda ya ziwa iliyoandaliwa na EWURA
Baadhi ya mafundi umeme wakiwa katika semina ya siku mbili mjini Shinyanga
Picha ya pamoja Mgeni  Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko  na mafundi umeme wa kanda ya Ziwa.

MKUU wa Wilaya ya Shinyanga Bi. Jasinta Mboneko, amewataka wananchi na taasisi zote wilaya ya Shinyanga mjini, kutumia mafundi umeme wenye leseni za EWURA, kufanya kazi za ufungaji wa mifumo ya umeme katika majengo yao.

Ameyasema hayo, leo Tar.12/10/2022 wakati akifungua semina ya siku mbili iliyoandaliwa na EWURA kwa mafundi umeme wa Kanda ya Ziwa, iliyofanyika katika ukumbi wa Shy- Park mkoa wa Shinyanga.

“Ninatoa agizo kwa taasisi na wananchi wa Shinyanga, kutumia mafundi umeme wenye leseni za EWURA, ili kuepuka madhara na majanga mbalimbali yanayoweza kutokea kwa kutumia vishoka”

Aidha, Mkuu wa Wilaya huyo alikabidhi leseni kwa fundi umeme Bw. Charles Jakson, aliyehudhuria semina hiyo na kupata leseni ya Daraja C ili kutoa hamasa kwa mafundi umeme wengine kuwa na leseni.

Akimkaribisha DC kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa EWURA, Meneja wa EWURA Kanda ya Ziwa, Bw. Geogre Mhina, alisema semina hiyo imelenga kuwafahamisha mafundi kuhusu Kanuni za Umeme( Ufungaji umeme majumbani) za Mwaka 2022, na namna ya kutumia mfumo wa maombi ya leseni za umeme (LOIS), unaopatikana katika tovuti ya EWURA(www.ewura.go.tz)

“Masuala mengine ni juu ya mfumo wa NIKONEKT kutoka TANESCO, mafunzo ya vitendo juu ya ukaguzi na kupima mitambo ya umeme

pia tutakusanya maoni juu ya bei elekezi kwa mafundi wa mifumo ya ufungaji umeme wa majumbani vijijini”alieleza Mhina.

Semina hii ya Sikumbili imehudhuriwa na mafundi zaidi ya 100 kutoka katika mikoa ya Shinyanga, Mwanza, Geita na Simiyu.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad