ALAF, TAASISI YA SARATANI OCEAN ROAD WAADHIMISHA MWEZI WA SARATASI KWA KUTOA ELIMU KWA WAFANYAKAZI - MTAA KWA MTAA BLOG

HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, October 18, 2022

ALAF, TAASISI YA SARATANI OCEAN ROAD WAADHIMISHA MWEZI WA SARATASI KWA KUTOA ELIMU KWA WAFANYAKAZI

Moja ya wafanyakazi wa Kampuni ya ALAF Limited, akichukuliwa damu kwaajili ya kupima kipimo cha Tezi dume. Ikiwa ni namna moja wapo ya kuadhimisha mwezi wa Saratani ya matiti ambayo hufanyika kila mwaka mwezi Oktoba. 

Meneja Uhusiano wa Kampuni ya ALAF Limited Hawa Bayumi akizungumza na waandishi wa Habari jijini Dar es Salaam leo wakati wa kuadhimisha Mwezi wa Saratani duniani. Ambapo mwezi huu wa Oktoba ni kwaajili ya Kutoa elimu kwa jamii ili kupima kabla madhara hayajaanza kuonekana.
Vipimo vikiendelea katika maadhimisho ya wiki ya saratani ya matiti.
Baadhi ya wafanyazi wa Kampuni ya ALAF Limited wakipata elimu juu ya Saratani.
Meneja Wa Kitengo cha Uchunguzi wa Saratani, Kutoka Taasisi ya Saratani Ocean Road, Dkt. Maguha Sephano akitoa elimu kwa wafanyakazi wa Kampuni ya ALAF Limited jijini Dar  Es Salaam leo Oktoba 18, 2022.
Meneja Uchunguzi ALAF, Willium Mhekela akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo. wakati wa kuadhimisha Mwezi wa Saratani Duniani ambao hufanyika Oktoba kila mwaka.
Meneja wa Masoko wa Kampuni ya ALAF Limited, Monica Mlalasi akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo. wakati wa kuadhimisha Mwezi wa Saratani Duniani ambao hufanyika Oktoba kila mwaka.
Meneja Wa Kitengo cha Uchunguzi wa Saratani, Kutoka Taasisi ya Saratani Ocean Road, Dkt. Maguha Sephano akizungumza na mwaandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo. mara baada ya kutoa elimu ya Saratani kwa wafanyakazi wa Kampuni ya ALAF Limited

KAMPUNI ya ALAF Limited imeadhimisha Mwezi wa Saratani ya Matiti kwa kutoa elimu ya Saratani ya kwa wafanyakazi wao wanaume na wanawake.

Meneja Uhusiano wa Kampuni hiyo, Hawa Bayumi akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo Oktoba 18, 2022. Amesema kuwa ALAF kwa kushirikiana na Taasisi ya Saratani Ocean Road wameadhimisha mwezi wa Oktoba wa Saratani ili wafanyakazi wote kupata elimu juu ya saratani ya matiti na kupata ufahamu zaidi juu Saratani nyingine zote.

"Elimu hii inayotolewa hapa Ofisini kwetu ni kwaajili ya Wanaume nawanawake wote ili kuwawekea mazingira ya wao kuweza kufanya vipimo na kujitambua mapema, kuangalia afya zao kwa ukaribu zaidi.

ALAF tunajali wafanyakazi wetu na wateja wetu, sisi tukiwa kwenye hali nzuri tunaweza kuwahudumia wateja wetu vizuri, kwahiyo kwa kujali kwetu tumeona upendo uanzie nyumbani, lakini pia tuweze kutuma ujumbe kwa watazania wote na ulimwenguni kote kuwa sisi tunajali na tupo pamoja nao wanaopambana na saratani." Amesema Hawa

Meneja Wa Kitengo cha Uchunguzi wa Saratani, Kutoka Taasisi ya Saratani Ocean Road, Dkt. Maguha Sephano amesema Taasisi ya Saratani mwaka huu imejikita katika kufanya uchunguzi wa saratani ya matiti kwani ikigundulika mapema inapona.

Amewaasa wananchi kufanya uchunguzi wa Mara kwa mara ili kuepusha kwenda hospitali pale ambapo mgonjwa anakuwa ameathirika sana na ugonjwa huo.

Amesema kuwa Takwimu za Mwaka jana taasisi ya Saratani Ocean Road, saratani iliyoongoza kwa wagonjwa wengi na kusababisha vifo vya wanawake wengi ilikuwa saratani ya Mlango wa Kizazi kwa asilimia 47.

"Inamaana kwamba Kati ya Wagonjwa 100 wenye Saratani 47 ni wagonjwa wa saratani ya Mlango wa Kizazi." Amesema

Amesema kwa Miaka ya hivi karibuni Saratani ya Matiti imekuwa ikiongezeka, kwa takwimu za mwaka jana taasisis hiyo ilipokea wagonjwa wapya 800, saratani hiyo inashika nafasi ya pili katika saratani zote.

"Saratani ya Matiti inakuja taratibu kutokana na dalili zake kuwa ni uvimbe ambao saa nyingine unaonekana na muda mwingine hauonekani. Kutokana na hilo tunatakiwa kuwaelimisha wananchi."

Kwa Upande wa wanaume amesema takwimu za mwaka jana zinaonesha Saratani ya Koo la Chakula inaongoza ikifuatiwa na saratani ya tezi dume.

Tunawahamasisha Wanaume kuwa na tabia ya kuchunguza afya zao hasa tezi dume kwani teknolojia ya upimaji imeongezeka na sasa wanapima kwa kuchukua damu.

Kwa Upande wake Meneja Uchunguzi ALAF, Willium Mhekela amewashukuru Wafanyakazi wa Kampuni ya ALAF kwa kushirikiana na Taasisi ya Saratani Ocean Road kwa Kwenda kutoa mafunzo ya Saratani kazini kwao ili waweze kujiepusha na Viatarishi kwa saratani.

"Nipo tayari Kupima Saratani kwa sababu tumepewa mafunzo ya kutosha." Amesema Mhekel

Ikumbukwe kuwa mwezi Oktoba kila Mwaka huwa ni mwezi wa maalumu kwaajili ya uelimishaji na mapambano ya saratani ya matiti duniani.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad