HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, September 12, 2022

TAASISI YA KUSAIDIA WATOTO YATIMA WENYE UMRI WA ZAIDI YA MIAKA 18 YAZINDULIWA LEO JIJINI DAR,

*TSO kutoa ujuzi kwaajili ya maendeleo ya watoto yatima
* Wahusika ni wale walio na umri wa miaka 18 na zaidi

TAASISI isiyo ya kiserikali ya Tanzanite Support Organization (TSO) imezinduliwa leo kwaajili ya kusaidia watoto yatima wanaofikisha miaka ya kuondoka katika vituo vya kulelea watoto yatima.

Akizungumza wakati wa uzinduzi huo, leo Septemba 12, 2022 Mkurugenzi wa Tanzanite Support Organization(TSO), Bahati Chando amesema kuwa lazima jamii ijiulize watoto wanaotoka katika vituo hivyo waenda wapi kipindi wanapofikisha miaka 18 ya kuondoka katika vituo hivyo.


Amesema kuwa taasisi hiyo itakuwa inamulika ndoto za watoto hao ili waweze kujisimamia katika kujipatia kipato chao wenyewe pindi tuu wanapofikisha umri wa kuondoka katika Vituo vya kulelea watoto yatima.

Amesema kuwa lengo la taasisi hiyo ni kuwawezesha watoto waliopo katika Makao ya kulelea watoto yatima ili waweze kujitegemea.

Kwa Upande wa Afisa Ustawi wa Jamii, Neema Mwalubilo amesema taasisi hiyo imefunguliwa kwa wakati muafaka sasa watakuwa na pa kuwapeleka watoto waliofikisha miaka 18 ili kwenda kupata ujuzi mbalimbali ili waweze kujikwamua katika maisha yao.

"Tulipopata barua kutoka taasisi hii tulifurahi kama Ustawi wa jamii kwasababu taasisi hii imekuja kwa wakati uliosahihi, huyu mtoto atakapopata elimu kutoka taasisi hii ya Tanzaniate Support Organization huyu mtoto ataweza kujitegemea na kuanzisha familia yake." Amesema Neema

Amesema kuwa Watoto wanaofikisha miaka 18 na kuendelea hawana haki ya kuoa wala kuolewa wakiwa kwenye makao, lakini wakitoka pale wanaweza kuoa na kuolewa kwani watakuwa wanajitegemea.

"Taasisi hii imekuja kutusaidia katika jambo ambalo tulikuwa tunahangaika nalo kwa muda mrefu."

Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa TPDC, Idris Hashim amesema amewashukuru TSO kwa kuwa na wazo la kuwasaidia watoto wanaofikisha miaka 18 na kuendelea ili kuwapa ujunzi ambao utawasaidia katika kujitegemea wao wenyewe.

Kwa upande wa wadau waliounga mkono juhudi za uanzishwaji wa taasisi hiyo wamesema taasisi hiyo isimamie malengo yake ili iweze kuwafikia vijana wengi zaidi. Pia amewaomba wadau waweze kujitoa kwaajili ya kuwapa elimu na ujuzi katika kuwatimizia malengo vijana hao wataokuwa wametoka kwenye makao ya kulelewa.
Mkurugenzi wa taasisi isiyo ya kiserikali ya Tanzanite Support Organization(TSO), Bahati Chando akizungumza wakati wa uzinduzi wa Taasisi ya kuwapa ujuzi watoto yatoma waliofikisha miaka 18 na kuendelea ili waweze kujitegemea wenyewe watokapo katika Vituo vya kulelea watoto yatima. Kulia ni Mkurugenzi wa LCC Solution Tz, Martin Brack na Kushoto ni Mkurugenzi wa kampuni ya Mind Garden Psychological Firm, Sumaiya Mahmoud.
 Afisa Ustawi wa Jamii, Neema Mwalubilo kulia akizungumza wakati wa Uzinduzi wa Kampuni ya kuwapa ujuzi watoto Yatima watokapo katika vituo vya malezi. Katikati ni Mkurugenzi wa LCC Solution Tz, Martin Black  na Mkurugenzi wa taasisi isiyo ya kiserikali ya Tanzanite Support Organization(TSO), Bahati Chando.
Mkurugenzi wa LCC Solution Tz, Martin Black akizungumza na wadau mbalimbali wakati wa uzinduzi wa taasisi ya kutoa ujuzi kwa watoto yatima waliofikisha miaka 18 na zaidi katika Makao, kulia ni Afisa Ustawi wa Jamii, Neema Mwalubilo  na kushoto ni Mkurugenzi wa taasisi isiyo ya kiserikali ya Tanzanite Support Organization(TSO), Bahati Chando.





Baadhi ya wadau wa kuendeleza watoto yatima waliofikisha umri wa kuondoka katika Makao wakizungumza jijini Dar es Salaam leo. Septemba 12, 2022.
Baadhi ya watoto Yatima waliofikisha umri wa kuondoka katika makao wakiwa katika uzinduzi wa taasisi ya kuwapa ujuzi ili waweze kujitegemea.
Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa TPDC, Idrisa Hashim Ramadhan akizungumza leo Septembe 12, 2022 wakati wa uzinduzi wa taasisi ya kukuza ujuzi wa watoto yatima waliofikisha umri wa kuondoka katika makao.
Picha ya pamoja.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad