Shabiki wa Simba na Manchester United ashinda Milioni 49.8 za 10Bet - MTAA KWA MTAA BLOG

HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, September 26, 2022

Shabiki wa Simba na Manchester United ashinda Milioni 49.8 za 10Bet


Na Mwandishi wetu

Dar es Salaam. Shabiki wa klabu ya Simba na timu ya Manchester United Derick Mustafa, ameshinda Sh49.8 milioni baada ya kubashiriki kwa kwa usahihi mechi 14 za ligi mbalimbali za soka duniani kupitia ‘mkeka’ wa kampuni ya 10 Bet.

Mustafa ambaye ni mkazi wa Kigamboni jijini Dar es Salaam alisema kuwa haikuwa kazi rahisi kushinda kiasi kikubwa cha fedha kutokana na kupata ugumu katika baadhi ya mechi zilizokuwa zinachezwa.

Alisema mechi iliyompa wakati mgumu zaidi ni kati ya Manchester United na Sheriff Tiraspol zilizokuwa zinacheza mchezo wa ligi ya Europa na Manchester United kuibuka washindi wa mabao 2-0 kwenye uwanja wa ugenini.

Kwa mujibu wa Mustafa, timu hizo hizo zilikuwa na uwiano sawa na alikuwa na wasiwasi wa timu yake kutokana na matokeo ya nyuma ambayo hayakuwa mazuri.

"Nilitumia uzoefu wangu katika kutabiri mechi hiyo na baadaye kupatia ambapo Manchester United ilishinda mabao 2-0. Nilifurahi kwani mbali yaushindi nimeweza kupata fedha kwa kupitia 10Bet,” alisema,” alisema Mustafa.

Alieleza kuwa fedha hizo atazitumia kuboresha biashara yake ndogo ya mtaji na kupanua mtandao wake wa masoko.

“Nitatumia fedha hizi kuanzisha na kuboresha miradi yangu mbalimbali ya ujasili amali. Ni faraja kwangu kushinda kiasi hiki kikubwa cha fedha. Lazima nichanganue aina ya biashara unayoenda kufanya, faida na changamoto zake kabla ya kuamua chochote,” alisema.

Meneja masoko wa 10Bet Tanzania George Abdulrahman alisema Mustafa anakuwa mshindi wa kwanza kujishindia mamilioni ya pesa kupitia kampuni yao.

Abdulrahman alisema 10BET ina bonasi kubwa zaidi barani Afrika yenye asilimia 1,000 ambayo inamwezesha mtu anayebashiri kushinda fedha nyingi zaidi kwenye ushindi wake.

“Mustafa alifanikiwa kuweka dau lake lililomwezesha kushinda Sh49.8m kupitia ‘bonus yetu ya ‘multibet’ ya asilimia elfu moja, tunatoa rai kwa watu wenye umri kuanzia miaka 18 kubashiri na 10bet ili kuweza kushindia fedha nyingi katika kupitia mkeka mmoja na zaidi. Unachotakiwa kufanya ni kutembelea www.10bet.co.tz, au kupitia app yetu na USSD *149*00#,  ” alisema Abdulrahman.

Meneja Masoko wa kampuni ya 10Bet, George Abdulrahman (Kushoto) akimkabidhi mfano wa hundi Derick Mustafa aliyeshinda Sh milioni 49.8 kwakubashiri kwa usahihi mechi 14 za ligi mbalimbali duniani kupitia mkeka wa 10Bet.

Meneja Masoko wa kampuni ya 10Bet, George Abdulrahman (Kulia) na mshindi wa Sh milioni 49.8 Derick Mustafa wakionyesha ishara ya ushindi baada ya hafla fupi ya makabidhiano.
No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad