RC SENYAMULE AAGIZA VIPINDI VYA DINI SHULENI VIIMARISHWE KUPUNGUZA MMOMONYOKO WA MAADILI - MTAA KWA MTAA BLOG

HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, September 14, 2022

RC SENYAMULE AAGIZA VIPINDI VYA DINI SHULENI VIIMARISHWE KUPUNGUZA MMOMONYOKO WA MAADILI

 

Mkuu wa mkoa wa Dodoma Rosemary Senyamule akihutubia katika maadhimisho ya miaka 75 ya utawa wa shirika la mtakatifu Gemma Galgani yaliyofanyika ukumbi wa Masista Kondoa Dodoma.

TAZAMA VIDEO HAPA CHINI
Mkuu wa mkoa wa Dodoma Rosemary Senyamule akiwa na baadhi ya viongozi wilaya ya Kondoa Dkt.Khamis Mkanachi katikati wakishiriki katika maadhimisho ya miaka 75 ya ya utawa wa shirika la mtakatifu Gemma Galgani yaliyofanyika ukumbi wa Masista Kondoa Dodoma.
Mkuu wa mkoa wa Dodoma Rosemary Senyamule akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi mbalimbali wa kanisa katoliki katika maadhimisho ya miaka 75 ya ya utawa wa shirika la mtakatifu Gemma Galgani yaliyofanyika ukumbi wa Masista Kondoa Dodoma.


Mkuu wa mkoa wa Dodoma Rosemary Senyamule akishiriki hafla fupi ya ukataji wa keki katika maadhimisho ya miaka 75 ya ya utawa wa shirika la mtakatifu Gemma Galgani yaliyofanyika ukumbi wa Masista Kondoa Dodoma.


Baadhi ya masista wakivishwa mataji kwa kutumikia kanisa kwa miaka mbalimbali tofauti kama sehemu ya pongezi katika utumishi.Na.Faustine Gimu Galafoni,Dodoma.
MKUU wa Mkoa wa Dodoma Rosemary Senyamule ametoa wito kwa taasisi za dini mkoani hapa kuendelea kutoa kipaumbele cha kufundisha masomo ya dini shuleni ili kuwajengea maadili mema watoto katika ulimwengu huu wenye mmomonyoko wa maadili.

Senyamule ametoa maelekezohayo leo Wilayani Kondoa mkoani Dodoma katika Maadhimisho ya miaka 75 ya utawa wa shirika la mtakatifu Gemma Galgani ambapo amesema kutokana na mmomonyoko wa maadili kuongezeka kwa vijana ni muhimu pia kwa viongozi wa dini kuchangamkia fursa ya kutoa elimu ya dini katika vipindi vya dini ambavyo vimetengwa katika vituo mbalimbali vya elimu kuanzia shule za msingi hadi vyuo vikuu.

“Niendelee kuwaomba taasisi za dini vipo vipindi vya dini serikali imetenga niendelee kuwaomba kufika katika shule mbalimbali kutoa elimu hii inayoendana na maadili ili kuwajenga watoto katika maadili kwani sisi ni mashahidi bado kuna mmomonyoko wa maadili katika nchi yetu”amesema.

Aidha, Senyamule ametoa wito kwa jamii kuendelea kushirikiana na taasisi za dini katika kusaidia makundi mbalimbali yaliyo katika mazingira magumu ikiwemo watoto yatima huku akisisitiza kuendelea kudumisha amani.

Hatua hiyo ya mkuu wa Mkoa imekuja mara baada ya utawa wa shirika la mtakatifu Gemma kuanzisha Mpango wa kusaidia watoto wa wazazi wafungwa.

“Mpango wa kuanzisha kituo cha kulea watoto wa wazazi walio katika magerezani ni kitendo kikubwa na cha muhimu sana hivyo nitoe wito kwa jamii kuendelea kushirikiana na taasisi za dini na serikali kwa ujumla kusaidia walio katika mazingira magumu”amesema.

Aidha,ametoa shukurani kwa taasisi za dini ikiwemo kanisa Katoliki kwa kuendelea kuwa mstari wa mbele kulinda amani.


Katika hatua nyingine mkuu huyo wa mkoa ametoa wito kwa wakazi mkoa wa Dodoma kuendelea kutunza mazingira hususan kuongeza mkazo wa upandaji miti ili kuifanya Dodoma ya Kijani.

Kuhusu suala la haki ,Senyamule amesema Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan imekuwa ni serikali ya kuheshimu haki na utawala wa kisheria.

Hata hivyo,amesema viongozi wa dini wamekuwa na mchango mkubwa katika uhamasishaji wa wananchi ushiriki wa sense ya watu na makazi 

“Zoezi la sense ya watu na makazi limekuwa na mafanikioa makubwa nah ii ni kutokana ninyi viongozi wa dini mmekuwa mkishirikiana na serikali katika kuhamasisha wananchi niwapongeze sana kwa kuleta ufanisi huo mkubwa”amesema.

Kwa upande wake Askofu mkuu mstaafu jimbo kuu la Dar Es Salaam Mwadhama Kadinali Pengo ametumia fursa hiyo kuwapongeza Masista kwa kutimiza miaka 75 huku akisisitiza kuwa sherehe za miaka 75 kwa shirika la Masister si mwisho wa dunia.

Hivyo,amehimiza kuendelea Kufanya kazi za utume kwa bidii.

"Shirika lenu lisipoteze dira na mwelekeo bali endeleeni Kufanya kazi ya utume kama shirika tutafungamana wote tu.

Askofu mkuu jimbo la Dodoma Beatus Kinyaiya ametoa wito kwa Masista kuendelea kuwa na mshikamano .

“Umoja na Mshikamano ni muhimu tuendelee kuwa wamoja kusaidia watu”amesema.

Hadi sasa jumla ya masisita 308 wameshahudumu utawa wa shirika la mtakatifu Gemma tangu kuanzishwa kwake mwaka 1947.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad