Benki ya Taifa ya Biashara
(NBC) imekutana na wateja wake wakubwa (Corporates) wa jijini Arusha ili
kujadili fursa za biashara, kutambulisha huduma mpya za benki hiyo
sambamba na kuwaejengea uelewa zaidi wateja hao kuhusu faida na manufaa
ya huduma hizo. Benki hiyo pia ilitumia fursa hiyo kujadiliana na wateja
hao namna inavyoweza kuboresha huduma zake kulingana na mahitaji yao.
Akizungumza
wakati wa mkutano huo wa asubuhi ‘Power breakfast business meeting’
ulioandaliwa na benki hiyo mapema hii leo jijini Arusha, Mkurugenzi wa
Wateja Wakubwa na Shughuli za Serikali wa NBC , Bw James Meitaron
aliemuwakilisha Mkurugenzi Mtendaji wa Benki hiyo Bw Theobald Sabi
alisema mkutano huo ni mwanzo wa mtiririko wa mikutano mingi kama hiyo
mahususi kwa wateja wakubwa katika mikoa mbalimbali hapa nchini ikiwemo
Mwanza, Dar es Salaam, Mbeya na Dodoma.
“Hatua hii ya kukutana na
wateja wetu wakubwa inatokana na maboresho makubwa tuliyofanya kwenye
huduma zetu ikiwemo kutambulisha huduma mpya zilizorahisishwa zaidi
kidigitali zinazoendana na mahitaji ya wateja wetu wakiwemo hawa
wakubwa. Tumeona tukutane nao ili tuweze kutambulisha kwao mapinduzi
haya kihuduma sambamba na kupokea mrejesho kutoka kwao kuhusu huduma
zetu,’’.
“Kupitia mpango huu pia tunapata fursa ya kuelezea
mikakati yetu mipana inayolenga kuwahudumia kwa ufanisi zaidi wateja
wetu, kuwasogezea huduma za kibenki karibu zaidi sambamba na kuwajengea
mitandao ya kibiashara miongoni mwao.’’
“Tunayafanya haya kwa
urahisi zaidi kwa kuwa sisi ni taasisi ya kifedha yenye uzoefu mkubwa
zaidi nchini huku tukiwa na mtandao mpana wa matawi, mawakala na huduma
za kidijitali. Uzoefu wetu sokoni unatupa faida ya kutoa huduma
zinaendana na mahitaji stahiki ya wateja wetu.’’ Alisema .
Alitaja
baadhi ya huduma zinazotolewa na benki hiyo kwa wateja wakubwa na
serikali kuwa ni pamoja na huduma za masoko ya fedha (financial
markets), usimamizi wa madeni (Dept management), mikopo ya mashirika
(corporate finance) pamoja na huduma za malipo ya serikali (GePG na
MUSE) ambapo benki hiyo inahudumia takribani asilimia10 ya makusanyo
yote ya serikali huku lengo likiwa ni kuhudumia makusanyo hayo kwa
asilimia 25 ifikapo mwaka 2025.
Kwa mujibu wa Bw Meitaron
miongoni mwa sekta muhimu ambazo benki hiyo imekuwa ikitoa kipaumbele ni
pamoja na miradi ya kimkakati ikiwemo miradi ya maliasili, miundombinu,
nishati, kilimo pamoja na miradi ya mawasiliano.
Akizungumzia
umuhimu wa hatua ya benki hiyo kukutana na wateja hao, Mkurugenzi wa
jiji la Arusha Bw Hargeney Chitukuro alisema hatua hiyo imekuja wakati
muafaka hasa katika kipindi hiki ambacho mkoa huo upo kwenye mapinduzi
makubwa ya kiuchumi kutokana ustawi mkubwa wa sekta ya utalii ikiwa ni
matunda ya jitihada za Rais Samia Suluhu Hassan kupitia mkakati wa Royal
Tour.
“Kwa sasa mkoa wa Arusha tupo kwenye kasi kubwa ya
mabadiliko ya kiuchumi yanayochagizwa na ukuaji wa sekta ya utalii,
biashara, kilimo na viwanda. Ni habari njema kwetu kuona kwamba benki ya
NBC ambayo inahudumia wadau wengi kwenye sekta hizi ikiwa ni pamoja na
wafanyakazi wa serikali wanatuunga mkono kupitia huduma zao za kisasa
ikiwemo zile za kidigitali ambazo kiukweli zimekuwa msaada mkubwa
hususani kwenye huduma za miamala ya kifedha na makusanyo ya serikali,’’
alisema.
Kwa upande wake mmoja wa washiriki wa mkutano huo Bi.
Jully Bede Lyimo kutoka Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA),
aliishukuru Benki ya NBC kwa kuandaa mkutano huo akionesha kuguswa na
maboresho makubwa ya kihuduma yanayoendelea kuoneshwa na benki hiyo huku
benki hiyo akiisihi kufanya uwekezaji zaidi katika sekta ya utalii.
"Napenda kuwashukuru uongozi wa Benki ya NBC kwa kuja na wazo zuri la
kukutana nasi, wateja wao, na kubadilishana maoni. Pia natoa wito kwa
Benki kuipa kipaumbele zaidi sekta ya utalii nchini na hivyo kuwafikia
kikamilifu na kutoa masuluhisho ya mahitaji ya kifedha ya wale walio
katika mnyororo wa thamani wa sekta hiki muhimu ya utalii,” alisema.
Mkurugenzi
wa wateja wakubwa na Shughuli za Serikali wa NBC , Bw James Meitaron
akizungumza na washiriki wa mkutano wa asubuhi unaofahamika kama ‘Power
breakfast business meeting’ ulioandaliwa na benki hiyo ili kujadili
fursa za biashara, kutambulisha huduma mpya sambamba na kuwaejengea
uelewa zaidi wateja hao kuhusu faida na manufaa ya huduma hizo. Mkutano
huo ulifanyika mapema hii leo jijini Arusha
Mkuu
wa Kitengo cha Uhusiano wa Benki ya NBC, Godwin Semunyu akizungumza na
washiriki wa mkutano wa asubuhi ‘Power breakfast business meeting’
ulioandaliwa na benki hiyo ili kujadili fursa za biashara, kutambulisha
huduma mpya sambamba na kuwaejengea uelewa zaidi wateja hao kuhusu faida
na manufaa ya huduma hizo. Mkutano huo ulifanyika mapema hii leo jijini
Arusha.
Meneja
wa Benki ya NBC Tawi la Arusha Bw Mirage Msuya akizungumza na
washiriki wa mkutano wa asubuhi ‘Power breakfast business meeting’
ulioandaliwa na benki hiyo ili kujadili fursa za biashara, kutambulisha
huduma mpya sambamba na kuwaejengea uelewa zaidi wateja hao kuhusu faida
na manufaa ya huduma hizo. Mkutano huo ulifanyika mapema hii leo jijini
Arusha
Sambamba
na kuwaejengea uelewa zaidi wateja hao kuhusu faida na manufaa ya
huduma za benki hiyo pia ilitumia fursa hiyo kujadili na wateja hao
namna inavyoweza kuboresha huduma zake kulingana na mahitaji yao.
Mkurugenzi
wa wateja wakubwa na Shughuli za Serikali wa NBC , Bw James Meitaron
(katikati walioketi) akiwa kwenye picha ya pamoja na maofisa wa benki
hiyo pamoja na washiriki wa mkutano wa asubuhi ‘Power breakfast
business meeting’ ulioandaliwa na benki hiyo ili kujadili fursa za
biashara, kutambulisha huduma mpya sambamba na kuwaejengea uelewa zaidi
wateja hao kuhusu faida na manufaa ya huduma hizo. Mkutano huo
ulifanyika mapema hii leo jijini Arusha
Friday, September 16, 2022

Benki Ya NBC Yakutana Na Wateja Wake Wakubwa wa Jijini Arusha.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment