HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, August 24, 2022

WADAU WA ELIMU WAITAKA AFRIKA KUWEKEZA ZAIDI SEKTA YA ELIMU

Washiriki kutoka nchi mbalimbali wakiwa katika picha ya pamoja na mgeni rasmi Naibu Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia, Mhe. Omary Juma Kipanga (katikati) na meza kuu kwenye afla ya ufungaji Mkutano wa Pili wa Kimataifa wa Elimu Bora (International Quality Education Conference -IQEC) kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Mwalimu Julias Nyerere.


 

Naibu Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia, Mhe. Omary Juma Kipanga (Mb) akizungumza alipokuwa akifunga Mkutano wa Kimataifa wa Elimu Bora uliomalizika juzi jijini Dar es Salaam, kujadili masuala anuai ya elimu kimataifa kwa lengo la kuboresha sekta hiyo.
Baadhi ya wanafunzi walioshiriki Mkutano wa Kimataifa wa Elimu Bora wakimkabidhi Naibu Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia, Mhe. Omary Juma Kipanga (katikati) risala yao mara baada ya kuisoma kwa washiriki wa mkutano huo. Kushoto ni Mratibu wa Taifa wa Mtandao wa Elimu Tanzania (TEN/MET), Bw. Ochola Wayoga akishuhudia.
Mratibu wa Taifa wa Mtandao wa Elimu Tanzania (TEN/MET), Bw. Ochola Wayoga akizungumza kwenye Mkutano wa Kimataifa wa Elimu Bora mbele ya mgeni rasmi Naibu Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia, Mhe. Omary Juma Kipanga.
Sehemu ya washiriki kwenye Mkutano wa Kimataifa wa Elimu Bora.
Mhadhiri Mkongwe, Dkt. Azaveli Lwaitama akichangia mada kwenye moja ya majadiliano katika Mkutano wa Kimataifa wa Elimu Bora uliofanyika jijini Dar es Salaam.
Na Joachim Mushi, Dar es Salaam
IMEELEZWA kuwa nchi za Afrika zinahitaji kufanya mabadiliko zaidi kwenye sekta ya elimu ikiwemo kufanya uwekezaji wa kutosha eneo hilo ili kupata matokeo chana yanayoweza kutatua changamoto zilizopo. Mabadiliko hayo yatafanikiwa endapo juhudi za pamoja zitafanywa na Serikali za mataifa husika wakiwemo wadau wa maendeleo, na wafadhili, waalimu, wanafunzi, wazazi na kila mmoja anayeguswa.

Kauli hii ni moja ya mapendekezo yaliotolewa na wadau wa elimu katika Mkutano wa Kimataifa wa Elimu Bora uliomalizika juzi jijini Dar es Salaam, kujadili masuala anuai ya elimu kimataifa kwa lengo la kuboresha sekta hiyo ya elimu.

Akizungumza na waandishi wa habari, Mratibu wa Taifa wa Mtandao wa Elimu Tanzania (TEN/MET), Bw. Ochola Wayoga ambao ni waratibu wa mkutano huo alisema wadau wamekubaliana kwa pamoja kuwa Bara la Afrika bado halijawekeza vya kutosha katika sekta ya elimu, hivyo kuzitaka Serikali na wadau wote kufanya uwekezaji wa kutosha ili kupata matokeo bora yatakayotatua changamoto zilizopo.

Alisema wajumbe katika mkutano huo wamezitaka asasi za kiraia kuwa kichocheo kuhakikisha Serikali za nchi zote duniani ikiwemo Tanzania zinatekeleza wajibu wake ipasavyo wa kuwekeza vya kutosha kwenye sekta ya elimu. "...Tunatambua kabisa kuwa dhamana ya kutoa elimu bora na jumuishi ambayo inakidhi mahitaji ya wanufaika wote ipo kwa Serikali," alisema Mratibu huyo wa TEN/MET.

Aidha aliongeza kuwa mkutano huo umebaini kuwa madhara ya COVID19 bado yapo sehemu mbalimbali barani Afrika hivyo ipo haja ya kuyafanyia kazi, mfano taifa kama Kenya lilifunga shule zake takribani mwaka mzima huku nchini Tanzania shule zikifungwa kwa miezi mitatu, hivyo itafutwe namna ya kufanyia kazi madhara hayo.

"...Na madhara ambayo tunayaongelea hapa ni kama ongezeko la watoto walioacha shule, kabla ya ujio wa COVID 19 walikuwa watoto milioni 258, baada ya COVID19 tunaongelea takribani watoto milioni 300, ambao kwa sasa hawako katika sehemu yoyote ya shule, tuna kila sababu kama wananchi na wadau kuhakikisha hawa watoto wanapata haki zao za msingi za shule," alisisitiza.

"Lingine ambalo tumelibainisha katika mkutano huu ni kwamba kuna haja ya kuwekeza katika elimu ya awali, Hii elimu ya awali kwa muda mrefu nchi hizi za Afrika ziliisahau kwa namna moja ama nyingine, tumepeana sasa majukumu," Bw. Wayoga akielezea maadhimio ya mkutano huo wa siku tatu wa kimataifa uliojadili masuala anuai ya elimu barani Afrika.

Mkutano huo wa Kimataifa wa Elimu Bora uliofanyia kwa siku tatu jijini Dar es Salaam, umekutanisha washiriki zaidi ya 300 kutoka mataifa 11 na kujadili masuala anuai ya elimu barani Afrika.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad