MKURUGENZI MKUU TCAA ACHAGULIWA MWENYEKITI MPYA AFPP - MTAA KWA MTAA BLOG

HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, August 23, 2022

MKURUGENZI MKUU TCAA ACHAGULIWA MWENYEKITI MPYA AFPP

 Mkurugenzi Mkuu Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA), Hamza Johari, amechaguliwa kuwa Mwenyekiti mpya wa Kamati ya Uboreshaji Miundombinu ya Usafiri wa Anga Angani(AFPP).

Uchaguzi huo umefanyika nchini Tanzania kwenye Mkutano wa AFPP katika kikao chake cha nane kilichofanyika Agosti 23, 2022 katika Ukumbi wa Kituo cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNICC),jijini Dar es Salaam. 
Mkurugenzi Mkuu anachukuwa nafasi hiyo kwa niaba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, nafasi ambayo ilikuwa inashirikiwa na Kenya kupitia kwa aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Kenya(KCAA), Kapteni Gilbert Kibe.
Akizungumza baada ya kuchaguliwa Mkurugenzi Mkuu TCAA Johari aliwashukuru wajumbe kwa kumchagua yeye binafsi na kuonyesha imani kwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa ujumla. Pia alimpongeza Mwenyekiti aliyemaliza muda wake Kapteni Kibe kwa kazi nzuri.
Mkurugenzi Mkuu TCAA alisema Mkutano huo wa siku mbili umelenga katika kujadili taratibu na njia za anga kwa bara la Afrika. Na kuongeza kuwa kwa utaratibu kila kiwanja cha ndege kina njia zake.
“Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni miongoni mwa nchi zenye njia za kisasa za anga na kutokana umahiri wetu Tanzania inasaidia pia nchi nyingine kutengeneza njia zao za kurukia”.alisema Mkurugenzi Mkuu TCAA.
Ameongeza pia kuwa unaweza ukawa na ndege nzuri lakini kama njia za angani sio nzuri inakuwa sio sawa. Amezitaja baadhi ya nchi Tanzania inazozisaidia kuwa ni Msumbiji, Eswatini na Senegali.
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania(TCAA), Hamza S.Johari akikaribishwa kuwa Mwenyekiti mpya wa Kamati ya Uboreshaji Miundombinu ya Usafiri wa Anga Angani(AFPP) katika kikao chake cha nane kilichofanyika Agosti 23, 2022 katika Ukumbi wa Kituo cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNICC),jijini Dar es Salaam. 
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania(TCAA), Hamza S.Johari akizungumza wakati wa kufungua mkutano wa Kamati ya Uboreshaji Miundombinu ya Usafiri wa Anga Angani(AFPP)  katika kikao chake cha nane kilichofanyika Agosti 23, 2022 katika Ukumbi wa Kituo cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNICC),jijini Dar es Salaam. 
Bw. Alfred Wagura akizungumza kwa niaba ya Mwenyekiti aliyemaliza Muda wake wakati wa kufungua mkutano wa Kamati ya Uboreshaji Miundombinu ya Usafiri wa Anga Angani(AFPP)  katika kikao chake cha nane kilichofanyika Agosti 23, 2022 katika Ukumbi wa Kituo cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNICC),jijini Dar es Salaam. 
Mwenyekiti mpya wa Kamati ya Uboreshaji Miundombinu ya Usafiri wa Anga Angani(AFPP) na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania(TCAA), Hamza S.Johari (wa pili kulia) akiongoza kikao cha kwanza mara baada ya kuchaguliwa kuwa mwenyekiti mpya kwenye kikao cha nane kilichofanyika katika Ukumbi wa Kituo cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNICC),jijini Dar es Salaam. 
Baadhi ya wajumbe Kamati ya Uboreshaji Miundombinu ya Usafiri wa Anga Angani (AFPP)  wakichangia mada kwenye kikao cha nane kilichofanyika katika Ukumbi wa Kituo cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNICC),jijini Dar es Salaam. 
Baadhi ya wajumbe Kamati ya Uboreshaji Miundombinu ya Usafiri wa Anga Angani (AFPP)  wakifuatilia mada kwenye kikao cha nane cha kamati hiyo kilichofanyika katika Ukumbi wa Kituo cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNICC),jijini Dar es Salaam. 
Mkuu wa Kitengo cha Taarifa za Usafiri wa Anga(TCAA) Hamis Kisesa akifafanua jambo kikao cha Kamati ya Uboreshaji Miundombinu ya Usafiri wa Anga Angani(AFPP) kilichofanyika katika Ukumbi wa Kituo cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNICC),jijini Dar es Salaam. 
Baaadhi ya Wajumbe wa Kamati ya Uboreshaji Miundombinu ya Usafiri wa Anga  Angani(AFPP) wakiwa kwenye picha ya pamoja kwenye kikao chake cha nane kilichofanyika kilichofanyika katika Ukumbi wa Kituo cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNICC),jijini Dar es Salaam. 
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania(TCAA), Hamza S. Johari akizungumza na waandishi wa habari kuhusu kikao cha Kamati ya Uboreshaji Miundombinu ya Usafiri wa Anga Angani(AFPP) kilichofanyika katika Ukumbi wa Kituo cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNICC),jijini Dar es Salaam. 
Mtaalamu wa Kutengeneza Miundombinu wa urukaji wa Ndege Angani/ Njia za Ndege Angani (TCAA), Peter Chinyama akizungumza na waandishi wa habari kuhusu namna wanavyoweza kutengeneza barabara za anga wakati wa  mkutano wa Kamati ya Uboreshaji Miundombinu ya Usafiri wa Anga Angani(AFPP) uliofanyika katika Ukumbi wa Kituo cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNICC),jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania(TCAA), Hamza S. Johari

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad