Benki ya NMB imetangaza
ushirikiano na kituo cha Radio cha EFM na TVE kama washiriki wenza
katika mbio za NMB Marathon 2022 zinazotarajiwa kufanyika Septemba 24,
2022 katika Viwanja vya Leaders Kinondoni jijini Dar es Salaam, huku
kauli mbiu ikiwa “Mwendo wa Upendo”.
Mbio hizo zenye lengo la
kurudisha tabasamu kwa akina mama wenye matatizo ya fistula kwa
kukusanya Sh. milioni 600 ambazo zitaenda kuwasaidia na matibabu katika
Hopsitali ya CCBRT.
Akizungumza jana katika uzinduzi huo
uliofanyika katika jengo la studio za EFM na TVE, Kaimu Mkuu wa Habari
na Mawasiliano kutoka NMB, Vicent Mnyanyika alisema kuwa katika marathon
iliyofanyika mwaka jana ambayo ilifanya vizuri hakukuwa na mshirika wa
chombo cha habari hivyo msimu huu tumeamua kushirikiana na kituo cha
radio cha EFM na TVE katika kukamilisha malengo ya kukusanya Sh. milioni
600.
“Mbio zetu zitakuwa za aina tatu kilometa 5, kilometa 10 na
kilometa 21 na gharama zake ni Tsh 20,000 kwa 5km, Tsh 20,000 kwa 10km
na Tsh 30,000 kwa 21km.Tukio letu litakuwa kuanzia asubuhi mpaka jioni,
baada ya kumaliza mbio, zawadi mbalimbali zitatolewa na kisha tuburudike
na wasanii mbalimbali,” alisema
Mkurugenzi wa Uendeshaji kutoka
EFM na TVE, Denis Busulwa (Ssebo) alisema furaha ya EFM na TVE kuendelea
kushirikiana na wadau mbalimbali katika kuinua masuala ya kijamii huku
akiamini ushirika wa EFM Na NMB ni ushirika mkubwa unaokutanisha chapa
(brand) bora katika kunyanyua masuala ya afya.
Tutakuwa na pre
party ya masaa 20 kuelekea siku ya Septemba 24, baada ya hapo washiriki
wote waliojisajili watapata nafasi ya kupata supu katika eneo hilo hilo
kwa pamoja kisha kuchukuliwa na basi litakalowapeleka mpaka katika
viwanja vya Leaders.
Jisajili na NMB Marathon kupitia https://marathon.nmbbank.co.tz/ uwe sehemu ya kurudisha tabasamu kwa akina mama wenye matatizo ya Fistula.

No comments:
Post a Comment