Mkuu
wa wilaya ya Mbeya, Mhe. Dkt Rashid Mohamed Chuachua akipokea mfano wa
hundi ya Shilingi Milioni 60 kutoka Meneja wa Benki ya NMB Kanda Nyanda
za Juu – Straton Chilongola akimwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, ikiwa
ni sapoti ya kuwezesha maonesho ya Nane Nane yanayofanyika Kitaifa
Mkoani Mbeya mwaka huu 2022
.
………………………………….
Benki ya NMB
imeendelea kuiunga mkono serikali katika kufanikisha maonyesho ya
Sikukuu ya Wakulima Kitaifa (Nanenane) kwa kukabidhi Sh. milioni 60 kwa
ajili ya maonyesho hayo.
Katika hafla ya kukabidhi hundi ya fedha
hizo iliyofanyika jana mjini Mbeya, Meneja wa NMB Kanda ya Kusini-
Straton Chilongola alisema kuwa benki hiyo imetoa kiasi hicho cha fedha
kwa ajili ya kufanikisha shughuli mbalimbali za maonyesho hayo.
Alisema
kuwa katika kipindi cha miaka mitano ambayo maonyesho ya Nane nane
yamekuwa yakifanyika, NMB imetoa udhamini wa zaidi ya Shilingi milioni
195 katika kufanikisha maonyesho hayo muhimu kwa Taifa.
Chilongola,
aliongeza kuwa katika kuunga mkono juhudi za Rais wa Awamu ya sita,
Samia Suluhu Hassan, Mchango wa NMB ni kujenga uchumi imara kupitia
kilimo na ufugaji ndani ya miaka minne kwani zaidi ya akaunti 644,034 za
wakulima zimefunguliwa nchi nzima.
Benki ya NMB inawakaribisha
Wananchi wote kutembelea banda lao katika Maonyesho ya Nanenane 2022
ndani ya Uwanja wa John Mwakangale mkoani Mbeya kupata masuluhisho yote
ya kifedha.
Tuesday, August 2, 2022

NMB YAKABIDHI MILIONI 60 MAONESHO YA NANENANE MBEYA
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment