HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, August 25, 2022

MAJESHI NCHI ZA AFRIKA KUTOA HUDUMA ZA AFYA BURE JIJINI DAR, PWANI NA ZANZIBAR, WANANCHI WAASWA KWENDA KUTIBIWA BURE

 

Kaimu Mkuu wa Operesheni na mafunzo wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi (JWTZ), Brigedia Generali, Charles Ndiege akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo Agosti 25, 2022.

JAMHURI ya Muungano wa Tanzania mwenyeji wa maadhimisho ya nne ya Majeshi ya nchi mwanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki yatakayoanza Agosti 26 hadi Agosti 31, 2022 nchini.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo Agosti 25, 2022, Kaimu Mkuu wa Operesheni na mafunzo wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi (JWTZ), Brigedia Generali, Charles Ndiege amesema kuwa maadhimisho hayo yataambatana na utoaji wa huduma za afya na kutoa misaada ya kibinadamu katika vituo mbalimbali vya Pwani, Dar  es Salaam na Zanzibar.

Amesema Maadhimisho hayo ya Majeshi ya nchi Mwananchama wa Afrika mashariki yataambana na kushirikiana na wananchi kwa kutoa huduma kwa jamii na kutoa misaada ya kibinadamu katika vituo vya kulelea Watoto na Wazee wenye mahitaji maalumu.

Amesema kuwa Wanajeshi Madaktari na wataalamu wa huduma za afya 190 kutoka nchi za Afrika Mashariki watatoa huduma kwa wananchi katika maeneo ya  Dar es Salaam, Pwani na Zanzibar.

Akizungumzia hospitali zitakazo toa huduma wakati wa maadhimisho hayo, Brigedia Generali Ndiege amesema hospitali ya Magomeni, hospitali ya Mbagala, Kituo cha Afya kigamboni, Kituo cha Afya Kibaha (Maili Moja), hospitali ya Bagamoyo na Kituo cha Afya cha Mpendaye Zanzibar ndivyo vitakavyotoa huduma ya afya na kinga kwa wananchi bila gaharama yeyote katika kuadhimisha ya Jeshi kushirikiana na wananchi. 

Brigedia Generali Ndiege amesema huduma huduma hizo zitakazotolewa bure kwa siku sita mfululizo kwa wananchi wa mikoa hiyo.

Aidha amewaomba wananchi kwenda kutibiwa katika hospitali zilizotajwa ili waweze kunufaika na huduma hizo.

"Majeshi yetu yatakabidhi vifaaa vya Ujenzi na Misaada ya kijamii katika vituo vya watoto na wazee wenye mahitaji maalumu."

Vituo vitakavyopewa misaada ni Kituo cha Watoto yatima cha Trust Group kilichopo Chamanzi, Hiari Orphans Centre Mbagala Rangi tatu na Makao Makuu ya Taifa ya watoto Kurasini.

Kwa upande wa Kigamboni ni Vituo vya Lady Fatima Orphanage Centre na Kituo cha Kiwahudumia watoto Nunge.

Kwa Bagamoyo misaada itatolewa katika kituo cha Watoto wa Moyo Mmoja na Kituo cha Watoto amani Orphanage Centre.

Kibaha Misaada hiyo itatolewa katika Kituo cha Watoto Sharom Orphan Centre Msangani na Kituo cha Watoto Buloma Foundation Children Picha ya ndege.

Brigedia Generali Ndiege amewaomba wananchi wanaoishi katika maeneo ya Dar es Salaam, Pwani na Zanzibar kujitokeza kwa wingi kuweza kupata huduma ya afya bila gharama yeyote inayotolewa na majeshi ya Afrika Mashariki.

Kwa Upande wa Mkuu wa Hospitali za Jeshi la Wananchi Tanzania(JWTZ) Brigedia Generali Dkt. Agatha Katua amesema kuwa huduma hizo zitatolewa bila kujali kuwa mgonjwa anaumwa ugonjwa gani na amesema matibabu yote yatafanyika katika vituo vilivyoainshwa na kutolewa dawa zote bila gharama yeyote. 

"Dawa na Vifaa tiba vyote vitatolewa bila gharama yeyote ili kila mwananchi anaufaike na huduma hizo zinazotolewa bure."

Aidha amewaomba wananchi kujitokeza ili kupata matibabu katika maeneo watakayokuwa wanatoa huduma hizo.

Majeshi hayo ya Nchi Mwananchama wa Afrika mashariki ni kutoka Rwanda, Burundi, Kenya, Uganda, Tanzani, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo na Sudani Kusini.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad