AMSHA AMSHA KUELEKEA CRDB BANK MARATHON 2022 - MTAA KWA MTAA BLOG

HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, August 4, 2022

AMSHA AMSHA KUELEKEA CRDB BANK MARATHON 2022

Ikiwa zimesalia siku chache kuelekea siku ya mbio za Kimataifa za CRDB Bank Marathon, uongozi wa klabu ya Yanga wakiongozwa na Mfadhili na Mdhamini Mkuu, Ghalib Salim Mohamed (GSM) na Rais wa Yanga, Hersi Said waliunga mkono kwa vitendo kwa kufanya mazoezi ya pamoja katika Amsha Amsha ya kuelekea Agosti 14.  Walianza kwa matembezi ya kutoka Makao Makuu ya Benki ya CRDB hadi viwanja vya The Green Oysterbay.
Hapo awali pia Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, AbdulMajid Nsekela akiambatana na Wakurugenzi Watendaji washirika wa CRDB Bank Marathon kufanya matembezi ya kujiweka sawa kulekea siku ya kilele ya mbio hizo, ambapo pia waliweza kusimika bendera ya CRDB Bank Marathon katika viwanja hivyo ambavyo mbio hizo zitaanza na kuishia.


 

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad