WAZIRI NAPE AELEZA UMUHIMU WA TCRA KUWA NA OFISI SABASABA - MTAA KWA MTAA BLOG

HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, July 6, 2022

WAZIRI NAPE AELEZA UMUHIMU WA TCRA KUWA NA OFISI SABASABA

 

Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Nape Nnauye akizungumza na waandishi wa habari wakati alipotembelea banda la Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA,) katika maonesho ya Sabasaba yanayoendelea jijini Dar es Salaam, Nape amepongeza utendaji kazi wa Mamlaka hiyo na kuitaka  kutoka na azimio la kujenga ofisi rasmi katika viwanja vya maonesho ya Sabasaba ili kuongeza kasi zaidi ya kuwahuduma wananchi pamoja na kukutana na wadau wa sekta hiyo.

Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Nape Nnauye (Kulia,) akizungumza na viongozi wa TCRA mara baada ya kutembelea banda la Mamlaka hiyo katika viwanja vya Sabasaba jijini Dar es Salaam. 


 
WAZIRI wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Nape Nnauye amepongeza utendaji kazi wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania  (TCRA,) na kuitaka  kutoka na azimio la kujenga ofisi rasmi katika viwanja vya maonesho ya Sabasaba ili kuongeza kasi zaidi ya kuwahuduma wananchi pamoja na kukutana na wadau wa sekta hiyo.

Nape ameyasema hayo leo mara baada ya kutembelea banda la TCRA katika maonesho 46 ya Kimataifa ya Biashara maarufu kama Sabasaba yanayoendelea jijini Dar es Salaam na kueleza kwa mahitaji ya watu kutoka TCRA ni makubwa na tayari ameongea na Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maendeleo Biashara nchini (TANTRADE,) Bi. Latifa Khamis juu ya Mamlaka hiyo kujenga ofisi katika viwanja hivyo ili kupunguza gharama sambamba na kuwa ofisi maalumu itakayowakutanisha na wa wadau wengi zaidi na kuwahudumia.

''Ninafurahi kuona TCRA ikikutana na wadau mbalimbali kutoka katika magazeti na redio na kuwahudumia pia wananchi wanafika hapa na kupata elimu kuhusiana na majukumu ya TCRA, kupitia maonesho haya ni vyema mkatoka na azimio la kujenga ofisi katika viwanja hivi vya maonesho...umuhimu wa TCRA ni mkubwa sana hasa katika mawasiliano ambayo yanamgusa kila mtanzania, kukiwa na ofisi hapa italeta nguvu zaidi katika kuwahudumia wananchi na kupunguza gharama za eneo hili ambalo TCRA inakutana na wadau wake na kutoa elimu kila mwaka.'' Amesema.

Waziri Nape amesema TCRA wamekuwa wakifuata kanuni na taratibu na kuzisimamia vyema katika kutoa huduma na kuwataka kuendelea na kasi hiyo kwa kuhakikisha watanzania wote wanapata huduma ya mawasiliano katika maeneo yote nchini.

Pia amesema kuwa katika maonesho hayo yanayokwenda na kauli mbiu ya 'Tanzania ni Sehemu Sahihi kwa Biashara na Uwekezaji'  ni fursa kwa waandishi wa habari kutangaza mambo makubwa yanayofanywa na Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan  ili kuvutia kampuni za uwekezaji na wafanyabiashara kwa manufaa ya taifa pamoja na kutumia fursa ya kampuni za nje zilizoshiriki maonesho hayo kwa kuzitangaza ili kuvuta wawekezaji wengi zaidi.Matukio mbalimbali wakati Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Nape Nnauye alipotembelea banda na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA,) katika maonesho ya Sabasaba yanayoendelea jijini Dar es Salaam.
 


 

 

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad