Ujumbe wa Unesco watembelea UDSM mradi wa CFIT lll - MTAA KWA MTAA BLOG

HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, July 8, 2022

Ujumbe wa Unesco watembelea UDSM mradi wa CFIT lll

 Na Mwandishi wetu

Mkuu wa Kitengo cha Elimu wa Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni la Umoja wa Mataifa nchini (UNESCO), Faith Shayo ameongoza ujumbe wa taasisi hiyo na washirika wengine kukagua utekelezaji wa mradi unaofadhiliwa na serikali ya watu wa China wa CFIT III unaoratibiwa na UNESCO katika Chuo Kikuu cha Dar es salaam.

Mradi CFIT wa miaka mitatu wenye lengo la kuboresha mausala, mitaala, mahusiano kati ya vyuo vikuu na sekta binafsi unaendeshwa katika taasisi zaidi ya 12 ikiwamo wizara inayohusika na elimu ya juu na ufundi.

Ujumbe huo ulioshirikisha UNESCO Makao Makuu nchini Ufaransa ulioongozwa na Mkuu Kitengo cha Elimu ya Juu  Bw. Peter Wells, Mratibu wa mradi wa CFIT III, Bi. Qinglin Kong, Mshauri wa Mradi wa CFIT III, Prof Tom Boland ulikutana na Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam (UDSM), Prof Bonaventure Rutinwa na kufanya kikao na wafanyakazi wa chuo, Wahadhiri pamoja na Wakuu vitengo mbalimbali wanaoratibu mradi huo

Katika mkutano huo mambo mbalimbali yalijadiliwa.

Kwa mujibu wa mkataba UNESCO wenye dhamana ya fedha za mradi huo za serikali ya watu wa China wanatakiwa kutembelea taasisi mbalimbali zilizomo katika mradi huo kufanya ukaguzi.

Ukaguzi kwa mwaka 2021 haukufanyika kutokana na kuwapo kwa ugonjwa  wa Uviko -19.

Ukaguzi huo umelenga kuboresha na kuimarisha ushirikiano kati ya wafadhili, watekelezaji na wizara husika katika utoaji wa elimu ya juu na ya ufundi.

Aidha umelenga kuangalia utekelezaji wa mradi katika vyuo husika na kuangalia namna ya kusaidia  kuleta ufanisi tarajiwa katika mradi kwa kutambua changamoto zilizopo na kuona maeneo ya kuboresha  kimenejimenti.

Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam (UDSM), Prof Bonaventure Rutinwa akizungumza na ujumbe wa UNESCO kutoka makao makuu ya Shirika hilo nchini Ufaransa alipotembelewa ofisini kwake ulioongozwa na Mkuu Kitengo cha Elimu ya Juu kutoka nchini Ufaransa makao makuu ya taasisi hiyo Bw. Peter Wells (wa tatu kushoto), Mratibu wa mradi wa CFIT III, Bi. Qinglin Kong (wa pili kulia), Mshauri wa Mradi wa CFIT III, Prof Tom Boland (wa tatu kulia) na mwenyeji wao Mkuu wa Kitengo cha Elimu wa Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni la Umoja wa Mataifa nchini (UNESCO), Faith Shayo (wa kwanza kulia) kwa lengo la kukagua maendeleo ya mradi wa CFIT III unaofadhiliwa na Serikali ya watu wa China na kuratibiwa na UNESCO. Wengine katika picha ni Mkurugenzi wa Elimu ya Juu - Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Dr. Kennedy Hosea (wa pili kushoto) na Mratibu wa Mradi wa CFIT III Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Prof Hannibal Bwire (wa tatu kulia)
Mkurugenzi wa Elimu ya Juu - Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Dr. Kennedy Hosea, Mratibu wa Mradi wa CFIT III Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Prof Hannibal Bwire pamoja na Wakuu wa vitengo mbalimbali wanaotekeleza wa mradi wa CFIT III chuoni hapo wakiwa kwenye mkutano na ujumbe wa UNESCO kutoka makao makuu ya Shirika hilo nchini Ufaransa  ulioongozwa na Mkuu Kitengo cha Elimu ya Juu kutoka nchini Ufaransa makao makuu ya taasisi hiyo Bw. Peter Wells, Mratibu wa mradi wa CFIT III, Bi. Qinglin Kong, Mshauri wa Mradi wa CFIT III, Prof Tom Boland na wakiambatana na mwenyeji wao Mkuu wa Kitengo cha Elimu wa Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni la Umoja wa Mataifa nchini (UNESCO), Faith Shayo kwa lengo la kukagua maendeleo ya mradi wa CFIT III unaofadhiliwa na Serikali ya watu wa China na kuratibiwa na UNESCO.
Mkuu Kitengo cha Elimu ya Juu  kutoka UNESCO makao makuu nchini Ufaransa Bw. Peter Wells akibadilishana uzoefu na timu ya wakuu wa idara mbalimbali wanaotekeleza mradi wa CFIT III katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (hawapo pichani) wakati wa zaiara ya kukagua maendeleo ya mradi wa CFIT III unaofadhiliwa na Serikali ya watu wa China na kuratibiwa na UNESCO.
Mratibu wa mradi wa CFIT III kutoka makao makuu ya UNESCO nchini Ufaransa Bi. Qinglin Kong akifafanua jambo  katika mkutano na wakuu wa vitengo mbalimbali wanaotekeleza mradi wa CFIT III chuoni hapo ( hawapo pichani) wakati wa ziara ya la kukagua maendeleo ya mradi wa CFIT III unaofadhiliwa na Serikali ya watu wa China na kuratibiwa na UNESCO.
Mkuu wa Kitengo cha Elimu wa Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni la Umoja wa Mataifa nchini (UNESCO), Faith Shayo akizungumza jambo katika mkutano na wakuu wa vitengo mbalimbali wanaotekeleza mradi wa CFIT III Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (hawapo pichani) wakati wa ziara ya la kukagua maendeleo ya mradi wa CFIT III unaofadhiliwa na Serikali ya watu wa China na kuratibiwa na UNESCO.
Baadhi ya wakuu wa idara mbalimbali wanaotekeleza mradi wa CFIT III Chuo Kikuu cha Dar es Salaam wakiwa kwenye mkutano na ujumbe wa UNESCO kutoka makao makuu ya Shirika hilo nchini Ufaransa waliofika chuoni hapo kukagua maendeleo ya mradi wa CFIT III unaofadhiliwa na Serikali ya watu wa China na kuratibiwa na UNESCO.
Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam (UDSM), Prof Bonaventure Rutinwa katika picha ya pamoja na ujumbe wa UNESCO kutoka makao makuu ya Shirika hilo nchini Ufaransa waliofika chuoni hapo kukagua maendeleo ya mradi wa CFIT III unaofadhiliwa na Serikali ya watu wa China na kuratibiwa na UNESCO. Wengine katika picha ni Mkurugenzi wa Elimu ya Juu - Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Dr. Kennedy Hosea, Mratibu wa Mradi wa CFIT III Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Prof Hannibal Bwire pamoja ugeni huo.No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad