KATIBU Tawala Uchumi na
Uzalishaji wa Mkoa wa Dar es Salaam, Dk Elizabeth Mshote ameipongeza
Kampuni ya Unilever ambayo ni watengenezaji wa Sabuni ya Omo kwa namna
ambavyo wamekua mstari wa mbele katika kushirikiana na Serikali katika
mambo ya kijamii.
Mshote ametoa pongezi hizo jijini Dar es Salaam
wakati wa uzinduzi wa muonekano mpya wa Sabuni ya Omo iliyoboreshwa
zaidi ambapo amesema Serikali itaendelea kuunga mkono juhudi za
wawekezaji wanaokuja kuwekeza nchini.
Dk Mshote amesema Kampuni
ya Unilever kupitia bidhaa yake ya Omo wamekua wadau wakubwa wa Serikali
na Watanzania kwa ujumla na kwamba anafarijika kuona wakizindua
muonekano mpya wa Sabuni hiyo.
" Wote tunatambua ya kwamba
Unilever ni kampuni kubwa na ya kimataifa ambayo bidhaa zake wengi wetu
humu hutumia kila siku. Kuna sabuni ambazo kila siku tunatumia kwenye
kufua, mafuta ambayo kila siku tunajipaka na royco ambayo ukitaka mboga
iwe tamu lazima tutumie.
Bidhaa za Unilever ni bidhaa zenye ubora
wa hali ya juu na zimekidhi vigezo vyote vya kimataifa. Ninayo furaha
kushiriki kwenye uzinduzi huu wa muonekano mpya wa sabuni ya Omo
iliyoboreshwa zaidi," Amesema Dk Mshote.
Amesema Unilever
Tanzania na Sabuni yao ya Omo wamekuwa Mstari wa Mbele katika kushiriki
mambo ya Kijamii katika mkoa wetu wa Dar es salaam hususani katika kutoa
Msaada wa Shuka Pamoja na sabuni kwenye Hospital zifuatazo Muhimbili
Hospitali, Mwananyamala Hospitali na Amana Hospitali.
Kwa upande
wake Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Unilever Tanzania, David Ninja
amemshukuru Katibu Tawala Uchumi na Uzalishaji Mkoa wa Dar es Salaam, Dk
Elizabeth Mshote kwa kufika kushiriki tukio hilo la uzinduzi wa
muonekano mpya wa Sabuni ya Omo ambapo pia amewahakikishia watanzania
kwamba ubora wa bidhaa hiyo umeongezeka maradufu.
" Kampuni ya
Unilever imekuwa ikienda sambamba na ukuaji wa teknolojia duniani ili
kuendana na hali ya soko na hususani kwa wateja wake.
hivyo leo
ni siku muhimu sana kwetu kwani tunazindua muonekano mpya wa sabuni ya
Omo iliyoboreshwa zaidi kwa lengo la kuendelea kuvutia watumiaji wa
sabuni hii.
Naomba nichukue fursa hii kuwaambia wateja wetu na
jamii ya Kitanzania kwamba ujumbe wetu kwa leo ni kuwa OMO NI MKALI WA
MADOA SUGU ni sabuni namba moja kwa kuondoa madoa sugu na kwa haraka
zaidi kwani unga na vimeng’enya viliyomo ndani mwake ni mzuri na huondoa
uchafu kwa haraka Zaidi na kuacha nguo yako ikiwa na harufu nzuri
(manukato) ndani ya siku 14," Amesema Minja.
Amesema Kampuni ya
Unilever kwa kupitia sabuni yake ya Omo imekuwa mstari wa mbele katika
kurudisha kile kidogo tupatacho kwa watanzania na kuungana na watanzania
katika kujenga Maisha bora kwa wote.
" Tumekuwa na kampeni
mbalimbali kama MKONO WA SHUKRANI, kwa mwaka jana, kampeni hii
ilifanyika katika Hospitali tatu jijini Dar es salaam Muhimbili,
Mwananyamala Pamoja na Hospitali ya Amana, ambapo tulichangia mashuka
Pamoja na sabuni kwa ajili ya watanzania wenzetu, Pia Omo tumekuwa na
kampeni ya Mkono Wa Ukarimu, kampeni maalum kabisa wakati wa kipindi cha
Mwezi Mtukufu wa Ramadhani kampeni hii ilifanyika na tulikusanya nguo
kutoka kwa watanzania wenzetu na tukafua kwa kutumia Omo na pia tukaenda
kuzikabidhi kwa wale watu wenye uhitaji," Amesema.
Pichani
kushoto ni Mgeni rasmi Katibu Tawala wa Uchumi na Uzalishaji Mkoa wa
Dar es Salaam Dkt Elizabeth Mshote pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa
Unilever Tanzania, David Minja kwa pamoja wakizindua muonekano mpya wa
sabuni ya OMO iliyoboreshwa zaidi kwenye hafla fupi iliofanyika jana
jijini Dar es Salaam.PICHA ZOTE NA MICHUZI JR-MMG.
Mgeni
rasmi Katibu Tawala wa Uchumi na Uzalishaji Mkoa wa Dar es Salaam Dkt
Elizabeth Mshote akizungumza mbele ya Wageni waalikwa mbalimbali
waliofika kwenye hafla ya uzinduzi wa muonekano mpya wa sabuni ya OMO
iliyoboreshwa zaidi uliofanyika jana jijini Dar es Salaam
Mkurugenzi
Mtendaji wa Unilever Tanzania, David Minja akizungumza mbele ya Wageni
waalikwa mbalimbali waliofika kwenye hafla ya uzinduzi wa muonekano mpya
wa sabuni ya OMO iliyoboreshwa zaidi uliofanyika jana jijini Dar es
SalaamSehemu ya Meza kuu akifuatilia yaliyokuwa yakijiri wakati wa uzinduzi wa muonekano mpya wa sabuni ya OMO iliyoboreshwa zaidi
Meneja
Masoko kampuni ya Unilever Tanzania,Upendo Mkusa akizungumza mbele ya
Wageni waalikwa mbalimbali waliofika kwenye hafla ya uzinduzi wa
muonekano mpya wa sabuni ya OMO iliyoboreshwa zaidi jana jijini Dar es
Salaam
Picha ya pamoja mara baada ya uzinduzi huo kufanyika
Msanii
wa muziki wa kizazi kipya (singeli) atambulikae kwa jina la kisanii
Shalo Mwamba akitumbuiza wageni waalikwa kwenye hafla hiyo
Mkurugenzi
Mtendaji wa Unilever Tanzania, David Minja akijiachia pamoja na msanii
Shalo Mwamba katika vionjo vya miondoko ya Singeli
Shalo Mwamba akitumbuiza kwenye hafla hiyoWageni waalikwa mbalimbali wakifuatilia yaliyokuwa yakijiri ukumbini humo
No comments:
Post a Comment