Afisa
Mtendaji Mkuu wa Benki ya NMB, Bi Ruth Zaipuna, ametunukiwa tuzo ya
heshima ya uongozi bora wa biashara barani Afrika kwa uongozi wake
shupavu wa taasisi hiyo kubwa ya fedha kuliko zote nchini Tanzania.
Ruth
Zaipuna ametunukiwa tuzo hiyo maalum ya “African Business Leadership
Commendation Award” ya mwaka 2022 na jarida la African Leadership kwa
juhudi zake za kuifanya Benki ya NMB kuwa mstari wa mbele katika ujenzi
wa taifa na kuchangia kikamilifu kuboresha maisha ya Watanzania.
Jarida
hilo linaloshapishwa na Taasisi ya African Leadership Organisation
yenye makao yake makuu huko London nchini Uingereza, lina ushawishi
mkubwa kimataifa na linaheshimika kwa kuyatangaza mafanikio ya bara la
Afrika duniani.
Kwa mujibu wa mwanzilishi na Mwenyekiti Mtendaji
wa taasisi hiyo, Dkt Ken Giama, sababu zilizofanya Bi Zaipuna kuibuka
kidedea ni pamoja na uongozi wake uliotukuka na kuifanya NMB kuwa kinara
wa ubunifu kwenye sekta ya benki nchini.
Dkt Giama alisema
zaidi ya kuwa kiongozi mahiri na mwenye msimamo thabiti wa kibiashara,
pia uongozi wake umechangia sana kusaidia NMB kutengeneza fursa nyingi
za ajira na kuzalisha mali nchini na barani Afrika kwa ujumla. Aidha,
aliongeza kuwa ushindi wa Bi. Zaipuna ulitokana na mchakato makini
unaozingatia sifa stahiki uliofanywa na timu ya uteuzi ya bodi ya
wahariri wa Taasisi hiyo.
Kiongozi huyo wa NMB alitunukiwa
heshima hiyo wakati wa kilele cha mkutano wa maendeleo ya Afrika na Tuzo
za Uongozi wa Biashara za Afrika (ABLA) zilizofanyika hivi karibuni
kwenye Ukumbi wa House of Lords katika Bunge la Uingereza.
Akizungumza
kabla ya kupokea zawadi ya Bi. Zaipuna wakati wa shughuli hiyo, Mkuu wa
Idara ya Teknolojia na Mabadiliko ya Kidijitali wa NMB, Bw Kwame
Makundi, alisema heshima hiyo ya kimataifa ina maana kubwa sana kwa
Benki ya NMB na Tanzania kwa ujumla.
Aliwaambia washiriki wa
hafla hiyo kuwa tuzo hiyo ni ushahidi wa juhudi za makusudi ambazo
uongozi wa Benki ya NMB umekuwa ukizingatia ili kuboresha maisha ya
Watanzania na kusaidia maendeleo ya taifa kwa ujumla.
Bi.
Zaipuna alisema katika hotuba iliyosomwa kwa niaba yake na Bw Makundi
kuwa tuzo hiyo haitambui tu mafanikio na mchango wake kama kiongozi bali
pia unatambua mchango wa Serikali ya Awamu ya Sita na Benki Kuu ya
Tanzania kuiwezesha NMB kustawi na kuendelea kuwanufaisha wadau wake
wote.
Taarifa kwa umma ya benki hiyo ilisema ushindi wa Bi
Zaipuna na washindi wenzake 10 wa tuzo za ABLA za mwaka huu
zilizofanyika Julai 10 pia ni matokeo ya umakini wao wa kibiashara na
mafanikio makubwa katika maendeleo ya sekta binafsi barani Afrika.
Mkutano
wa Afrika ni moja ya programu muhimu za jarida la African Leadership
unaowaleta pamoja viongozi wa taasisi za umma na sekta binafsi kutoka
Afrika, Ulaya na Marekani kwa lengo la kujadili masuala mbalimbali kwa
ajili ya mustakabli mpya wa bara hili na ulimwengu wote.
Taarifa
iliyotolewa kwenye vyombo vya habari jana, inaonyesha kuwa mbali na Bi
Zaipuna, wengine walioshinda tuzo za ABLA zilizotolewa Julai 4, 2022 ni
Mfanyabiashara na Bilionea wa Lesotho Sam Matekane aliyeshinda tuzo ya
heshima ya Maisha, Waziri wa Fedha wa Mauritius Dr Renganaden Padayachy,
tuzo ya Kiongozi bora wa Biashara Afrika ilienda kwa Mwenyekiti wa
Mtandao wa Mitaji Nigeria Dr. Akintoye Akindele, Afisa Mtendaji Mkuu wa
United Capital Plc ya Nigeria Mr Peter Ashade alishinda Afisa Mtendaji
Mkuu wa Mwaka 2022.
Afisa Mkuu wa Teknolojia na Mabadiliko ya Kidijitali wa NMB - Kwame
Makundi (kushoto)akimkabidhi tuzo ya Uongozi wa Biashara Barani Afrika
mwaka 2022 - Afisa Mtendaji Mkuu wa NMB - Ruth Zaipuna. Bi Ruth
alitunukiwa tuzo hiyo na Jarida la African Leadership katika hafla
iliyofanyika jijini London kwenye ofisi za Bunge la Uingereza juzi na
kuwakilishwa na Bwana Kwame Makundi. Tuzo hiyo imemtambua Bi Zaipuna
kama kiongozi shupavu na mahiri kwa uongoza wake na ubunifu katika sekta
ya benkiAfisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya NMB – Ruth Zaipuna qkipongezwa na wafanyakazi wa NMB baada ya kukabidhiwa tuzo.
Afisa
Mkuu wa Teknolojia na Mabadiliko ya Kidijitali wa NMB - Kwame Makundi
akipokea tuzo maalum ya Uongozi wa Biashara Barani Afrika mwaka 2022
kutoka kwa Waziri wa Biashara Ofisi ya Waziri Mkuu wa Uingereza - Lord
Dollar Popat kwa niaba ya Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya NMB – Ruth
Zaipuna. Bi Ruth alitunukiwa tuzo hiyo na Jarida la African Leadership
katika hafla iliyofanyika jijini London kwenye ofisi za Bunge la
Uingereza juzi na kuwakilishwa na Bwana Kwame Makundi. Tuzo hiyo
imemtambua Bi Zaipuna kama kiongozi shupavu na mahiri kwa uongoza wake
na ubunifu katika sekta ya benki.
Tuesday, July 12, 2022

Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya NMB atunukiwa Tuzo ya Uongozi Bora wa biashara Afrika
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment