*Yakutana na wasambazaji wake kupanga mikakati ya ushirikiano
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Mbolea ya Yara Tanzania, Winstone
Odhiambo ( kulia ) akikabidhi mfano wa hundi yenye thamani ya shs
58,879,945.84 kwa mshindi wa kwanza, Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya
Hapco Agrobusiness, Conrad Alex ( katikati) baada ya kuibuka mshindi kwa
kufanya mauzo mengi zaidi wakati wa mkutano wa mwaka wa wasambazaji wa
kampuni hiyo jijini Dar es Salaam jana.
Mkurugenzi
Mtendaji wa Kampuni ya Mbolea ya Yara Tanzania, Winstone Odhiambo (
kulia ) akikabidhi mfano wa hundi yenye thamani ya shs 27,321,514.80 kwa
mshindi wa tatu, Mkurugenzi Msaidizi wa Kampuni ya Mtewele General
Traders, Deogratius Mtewele ( wa pili kushoto ) baada ya kuibuka mshindi
kwa kufanya mauzo mengi zaidi wakati wa mkutano wa mwaka wa wasambazaji
wa kampuni hiyo jijini Dar es Salaam jana.
Mkurugenzi
Mtendaji wa Kampuni ya Mbolea ya Yara Tanzania, Winstone Odhiambo (
kulia ) akikabidhi mfano wa hundi yenye thamani ya shs 52,674,275.28 kwa
mshindi wa pili, Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Nasa Kilimo, Nasa
Mhina ( wa pili kushoto ) baada ya kuibuka mshindi kwa kufanya mauzo
mengi zaidi wakati wa mkutano wa mwaka wa wasambazaji wa kampuni hiyo
jijini Dar es Salaam jana.
Mkurugenzi
Mtendaji wa Kampuni ya Mbolea ya Yara Tanzania, Winstone Odhiambo (
kushoto ) akizungumza na washiriki wa mkutano wa mwaka wa wasambazaji wa
kampuni hiyo jijini Dar es Salaam jana. Mkutano huo ulijadili jinsi ya
kukuza ushirikiano kwa manufaa ya pande zote mbili.
Kaimu Meneja Idara ya Uzalishaji wa kampuni ya Mbolea ya Yara Tanzania,
Frank Lugoba ( kushoto ) akizungumza na wasambazaji wa kampuni hiyo
wakati wakitembelea katika kiwanda cha Yara, jijini Dar es Salaam jana.
Wasambazaji hao kutoka maeneo mbalimbali nchini walikuja kushiriki
mkutano wa mwaka wa kujadili jinsi ya kukuza ushirikiano kwa manufaa ya
pande zote mbili
Bwanashamba
Mwandamizi Mstaafu wa Kampuni ya Mbolea ya Yara Tanzania, Maulidi Mkima
( kulia ) akizungumza na wasambazaji wa kampuni hiyo wakati
wakitembelea kiwandani hapo jijini Dar es Salaam juzi. Wasambazaji hao
kutoka maeneo mbalimbali nchini walikuja kushiriki mkutano wa mwaka wa
kujadili jinsi ya kukuza ushirikiano kwa manufaa ya pande zote mbili.
Mkurugenzi
Mtendaji wa Kampuni ya Obo Investment, Olais Oleseenga akiuliza swali
wakati wa mkutano wa mwaka wa wasambazaji wa kampuni hiyo jijini Dar es
Salaam jana. Mkutano huo ulijadili jinsi ya kukuza ushirikiano kwa
manufaa ya pande zote mbili kwa msimu wa mwaka 2021/22.
Meneja wa Uagizaji na Uuzaji Nje wa Mamlaka ya Udhibiti wa Mbolea
Tanzania (TFRA), Louis Kasera akizungumza na washiriki wa mkutano wa
mwaka wa wasambazaji wa kampuni hiyo jijini Dar es Salaam jana. Mkutano
huo ulijadili jinsi ya kukuza ushirikiano kwa manufaa ya pande zote
mbili.
Wafanyakazi
na wasambazaji wa kampuni ya Mbolea ya Yara Tanzania, wakiselebuka
kuhitimisha mkutano wao wa mwaka jijini Dar es Salaam jana.
Saturday, July 30, 2022

kampuni ya Yara Tanzania yawatoa hofu wakulima upatikanaji wa mbolea msimu wa Kilimo.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment