HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, July 28, 2022

BODI YA TUME YA TAIFA YA UMWAGILIAJI YABARIKI MPANGO MKAKATI WA TUME NA UTEKELEZAJI WA BAJETI YA MWAKA 2022 – 2023

 

 Wajumbe wa bodi ya tume ya Taifa ya Umwagiliaji wameupitia na kupitisha mpango mkakati wa Tume ya Taifa ya Umwagiliaji ikiwemo kubariki matumizi ya Bajeti ya Taasisi hiyo ya zaidi ya Shilingi Bilioni 366 kwa Mwaka wa fedha 2022 – 2023.


Akizungumza katika kikao hicho Mwenyekiti wa Bodi Prof. Henry Mahoo ameitaka Menejimenti ya Tume ya Taifa kufanya kazi kwa ushirikiano na weledi ili kufanikisha utekelezaji wa Bajeti na miradi iliyoainishwa kujengwa kwa mwaka wa fedha 2022 – 2023 kwa weledi na kiwango stahiki.

Bodi hiyo imepata fursa ya kutembelea mradi wa jengo la Makao Makuu ya Tume linalojengwa eneo la Njedengwa jijini Dodoma.Wajumbe wa bodi wamerizishwa na kazi inayoendelea ambapo wameshauri wahusika katika usimamizi na ujenzi wa jengo hilo kwa mtindo wa (Force account) kuboresha uhifadhi wa kumbukumbu na nyaraka za ujenzi wa jengo hilo. Awamu ya kwanza ya ujenzi wa jengo hilo la Makao Makuu ya Tume utagharimu jumla ya Tshilingi Bilioni 1.7 ambapo utafuatiwa na mpango wa awamu ya pili utakaowezesha jengo hilo kuwa na Gorofa 4.

Kikao cha bodi pia kimehusisha ziara ya kutembelea Skimu ya kilimo cha Zabibu ya Chinangali na Hombolo.Wakiwa katika Skimu ya Chinangali wajumbe wa Bodi ya Tume wameshauri wakulima wa Skimu hiyo kujifunza teknolojia mpya,rahisi na zenye unafuu kwa shughuli za kilimo cha umwagiliaji ili kupunguza gharama za uwekezaji katika kilimo hicho. Skimu ya kilimo cha zabibu Chinangali ina jumla ya Heka 295 zinazoendelea kufufuliwa na Wizara ya Kilimo chini ya Tume ya Taifa ya Umwagiliaji.

Kwa mujibu wa Mhandisi wa Umwagiliaji wa Mkoa wa Dodoma Raphael Laizer ameahidi kuufanyia kazi ushauri ulitolewa na wajumbe wa bodi, kazi zilizofanyika katika Skimu hiyo ni pamoja ununuzi wa mipira ya mashambani(Drip lateral pipe) vifaa vya kufungua na kufunga mifumo ya umwagiliaji (Control valve system) pamoja na ukarabati wa jengo la pampu ya kuvuta na kusambaza maji.

Mhandisi laizer ameendelea kusema kuwa ujenzi wa mradi huo umefikia asilimia 25, ambapo utatumia zaidi ya Shilingi Milioni Mianne Sitini na Nane(468,000,000/=) hadi kukamilika mwishoni mwa mwaka huu.

Katika Skimu ya Zabibu ya Hombolo wajumbe wametembele Bwawa la Umwagiliaji na kugundua mapungufu katika utunzaji wa mazingira ambapo wameagiza kitengo cha Mazingira kuratibu utunzanji wa Mazingira katika tuta la Bwawa hilo sanjari na kuzuia uharibifu wa mazingira unaofanywa na binadamu kandokando ya Bwawa hilo.

Katika hatua nyingine Wajumbe wa Bodi ya Tume wameishauri Tume ya Taifa ya Umwagiliaji kufanya utafiti wa udongo na maji ili kugundua chanzo cha uharibifu wa miche ya Zabibu katika baadhi ya mashamba ya Skimu hiyo.

Wakulima katika Skimu hiyo wameitikia wito wa serikali wa kuongeza bidii katika kilimo cha Zabibu ambapo kwa sasa wanavuna hadi tani Nane (8) kwa Heka mmoja lakini wanakabiliwa na changamoto ya ukosefu wa masoko, wameiomba serikali iwasaidie katika ujenzi wa viwanda vya kuchakata mchuzi wa Zabibu suala litakalo imarisha mapato ya zao hilo.Wajumbe wa Bodi ya Tume na Menejimenti ya Tume ya Taifa ya Umwagiliaji wakikagua miche ya Zabibu iliofifia ubora katika Skimu ya Zabibu ya Hombolo.

Wajumbe wa Bodi ya Tume ya Taifa ya Umwagiliaji katika kikao cha kubariki matumizi ya Bajeti ya Mwaka 2022 – 2023 jijini Dodoma.

Ujenzi wa jengo la Ofisi za Tume Makao Mkuu eneo la Njedengwa jijini Dodoma.


No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad