HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, June 2, 2022

WANAFUNZI WATANZANIA WANUFAIKA NA FURSA ZA MASOMO UFARANSA

  

BALOZI wa Ufaransa nchini Tanzania Nabil Hajlaoui amesema katika kuendeleza mahusiano mazuri na Tanzania wataendelea kuongeza idadi ya wanafunzi wa kitanzania watakakwenda kusoma masomo ya shahada za Awali, shahada za Umahiri na Uzamivu nchini Ufaransa ili kitimiza azma ya kubadilishana Teknolojia na ubunifu baina ya nchi hizo.

Ameeleza hayo wakati hafla ya dhifa iliyowakutanisha wanafunzi waliowahi kusoma nchini Ufaransa (Alumni,) pamoja na wanafunzi watatu waliopata ufadhili wa masomo nchini Ufaransa kuanzia mwezi Septemba.

Balozi Nabil amesema wanafunzi watanzania watumie fursa hiyo ili kuleta tija kwa Taifa.

"Serikali ya Tanzania imejikita katika uwekezaji na Rais Samia Suluhu Hassan na Rais wa Ufaransa wamedhamiria hilo mara baada ya kukutana na wawekezaji kutoka Ufaransa wameshaanza kuja Tanzania kupitia kampuni kubwa na za kati ambazo zinahitaji wataalamu... wanafunzi wafuatilie fursa hizi za masomo ambayo watayasoma kwa kiingereza na waweke nia katika hilo.

Balozi Nabil amesema, wamekuwa wakitembelea vyuo mbalimbali nchini na kueleza fursa mbalimbali za masomo na ujuzi wanazoweza kuzipata kupitia ubalozi wa Ufaransa nchini.

Mmoja ya wanufaika wa fursa ya masomo Mathew Choaji ambaye atakwenda kusomea masuala ya dawa na Vifaa Tiba amesema, fursa hiyo italeta tija kwa jamii hasa katika sekta ya afya.

Amesema, kwa wakati huu ambao Serikali imejikita katika uwekezaji ikiwemo ujenzi wa viwanda vya dawa italeta wataalamu wazawa katika kuviendesha kwa faida ya watanzania. 

Mtandao wa Alumni wa Ufaransa una zaidi ya wahitimu wapatao 340,000 waliojisali kote duniani huku Tanzania ikiwa na wanachama 400 waliosajiliwa kupitia Tanzania Francealumni.

 Balozi wa Ufaransa nchini Tanzania Nabil Hajlaoui akizungumza wakati wa hafla ya doing iliyowakutanisha wanafunzi watanzania waliowahi kusoma nchini Ufaransa pamoja na wanafunzi watatu waliopata ufadhili wa masomo nchini Ufaransa kuanzia mwezi Septemba mwaka huu, Balozi ameeleza kuwa wataendelea kuongeza idadi ya watanzania watakaokwenda kusoma nchini Ufaransa.


Balozi wa Ufaransa nchini Tanzania Nabil Hajlaoui akizungumza wakati wa hafla ya doing iliyowakutanisha wanafunzi watanzania waliowahi kusoma nchini Ufaransa pamoja na wanafunzi watatu waliopata ufadhili wa masomo nchini Ufaransa kuanzia mwezi Septemba mwaka huu, Balozi ameeleza kuwa wataendelea kuongeza idadi ya watanzania watakaokwenda kusoma nchini Ufaransa.
Mwanafunzi aliyepata fursa ya masomo nchini Ufaransa Mathew Choaji akizungumza wakati wa hafla hiyo na kuahidi kuitumia vyema fursa hiyo kwa manufaa ya jamii.
Matukio mbalimbali yakiendelea wakati wa hafla hiyo.
 


No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad