HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, June 6, 2022

WAHANDISI KILIMO CHA UMWAGILIAJI WATAKIWA KUSIMAMIA UJENZI NA UKARABATI WA MIUNDOMBINU KWA UMAKINI

 




Kaimu Mkuregenzi Idara ya Miundombinu kutoka Tume ya Taifa ya Umwagiliaji Mhandisi Ntonda Kimasa mwenye kofia nyeupe, akitoa maelekezo kwa msimamizi wa mradi wa ukarabati wa skimu ya Idudumo Mhandisi Jumbe Tibori mwenye kofia nyekundu kushoto, wakati wa ukaguzi wa kazi inayoendelea katika skimu hiyo.



Picha ikionesha sehemu ya mfereji mkuu wenye urefu wa kilomita mbili utakaopeleka maji mashambani ukiwa katika atua ya ujenzi.

(Habari na Picha na Kitengo cha Habari na Mawasilino.)




NZEGA - TABORA


Wahandisi wa Kilimo cha Umwagiliaji nchini wametakiwa kusimamia kazi za ujenzi na ukarabati wa miundombinu ya kilimo cha umwagiliaji katika maeneo ya miradi kwa umakini na ueledi mkubwa kwani, kazi hizo zinatakiwa kufanyika kwa wakati kulingana na mkataba kwa wakandarasi na hakutakuwa na muda wa nyongeza kwa mkandarasi ambaye atafanya kazi kwa kuchelewa na chini ya kiwango.

Hayo yameelezwa mwishoni mwa wiki, na Kaimu Mkureugenzi wa Idara ya Miundombinu kutoka Tume ya Taifa ya Umwagiliaji, Mhandisi Ntonda Kimasa, alipokuwa katika skimu ya Kilimo cha Umwagiliaji Idudumo wilayani Nzega Mkoani Tabora.

Mhandisi Kimasa alisema, Serikali imewekeza zaidi ya shilingi milioni 700 fedha za ndani, kwa ajili ya utekelezaji wa mradi huo ambao una bwawa na utahusisha kuboresha mfereji mkubwa wenye urefu wa kilimita mbili pamoja na mifereji mingine mitano ya upili ya kupeleka maji mashambani.

Baada ya kufanya ukaguzi wa ujenzi na ukarabati katika skimu hiyo Mhandisi Kimasa alisema “Kwa ujumla kazi inaendelea vizuri na ninaamini kazi itakamilika na mkandarasi ataikabidhi kwa wakati.” Alisisitiza.

Akiongea kwa niaba ya wakulima wa chama cha umwagiliaji Idudumo, Bwana Stefano Honoli ambaye pia ni mjumbe wa kamati ya ujenzi, amemshukuru Mbunge wa Nzega Mhe. Hussein Bashe ambaye pia ni Waziri wa Kilimo, kwa jitihada anazofanya katika kuboresha sekta ya kilimo cha umwagiliaji na kuiomba serikali ya awamu ya sita kuendelea na awamu nyingine ya ukarabati katika skimu hiyo kwa kutoa mafungu zaidi ya fedha, kwani skimu hiyo inauwezo wa kulisha mkoa mzima wa Tabora.

Kazi ya ukarabati wa skimu ya kilimo cha umwagiliaji Idudumo inayofanywa na mkandarasi mzalendo M/S Explicit Main Constractors Ltd. inategemewa kukamilika mwezi wa kumi mwaka huu, na utasaidia wakulima kufanya shughuli za kilimo cha umwagiliaji katika kipindi chote cha mwaka.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad