HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Saturday, June 18, 2022

WADAU WA MAGONJWA YA AFYA YA AKILI WAKUTANA WAJADILI MATOKEO YA AWALI YA 'KUPAA'

 

Mganga Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Dk Rashid Mfaume akizungumza wakati wa kufungua kikao cha kutoa matokeo ya awali ya utafiti wa KUPAA katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili wakati wa uwasilishaji matokeo ya awali ya utafiti wa KUPAA uliofanyika katika mikoa ya Dar es Salaam na Mbeya
Muuguzi Mstaafu wa Magonjwa ya afya ya Akili katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Karina Mabuja akizungumza na waandishi wa habari leo Juni 117, 2022 katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili wakati wa uwasilishaji matokeo ya awali ya utafiti wa KUPAA uliofanyika katika mikoa ya Dar es Salaam na Mbeya.
Mkuu wa Idara ya maadili ya tafiti za Afya wa Taasisis ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (NIMR), Daktari Otilia Flavian akizungumza leo Juni 117, 2022 katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili wakati wa uwasilishaji matokeo ya awali ya utafiti wa KUPAA uliofanyika katika mikoa ya Dar es Salaam na Mbeya.

Baadhi ya wadau wa magonjwa ya Afya ya akili wakiwa kwenye kikao hicho jijini Dar es Salaam.

WADAU wa afya ya akili wakutaka katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kwaajili ya kutoa matokeo ya awali ya utafiti wa KUPAA.

Akizungumza na waaandishi wa habari jijini Dar Es Salaam leo Juni 17, 2022 Muuguzi Mstaafu wa Magonjwa ya afya ya Akili katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Karina Mabuja amesema kuwa Utafiti huo wa awali umefanyika katika mikoa miwili wa Dar es Salaam na Mbaya na ameeleza maana ya KUPAA kuwa ni kuwezeshana kupata Uzima kwa watu wenye magonjwa ya Afya ya Akili.

Amesema kuwa kumekuwa na Changamoto nyingi kwa. Wagonjwa wa akili hasa wale wenye magonjwa ya afya akili sugu, waliona ni mhimu kukaa na kujua mahitaji ya wagonjwa na kuangalia namna ya kutatua changamoto hiyo.

"Tunafahamu kuwa wanatumia dawa ni kweli dawa inatuliza ugonjwa lakini mgonjwa anatakiwa mambo mengine kwenye jamii kama kushirikiana na jamii kama binadamu anavyotakiwa awe anafanya katika jamii pamoja na shughuli za Familia.

Karina amesema kuwa katika utafiti huo wa awali ulikutanisha wataalamu wa Afya, Madaktari, wauguzi Viongozi wa Afya, Serikali pamoja na wadau mbalimbali waliopo kwenye jamii kama vile waganga wa Jadi, tiba za kiroho, watu wa tiba ya kiislam, Mashekhe, wachungaji na wale wanaokaa na wagonjwa wenye matatizo ya afya ya akili.

Amesema kuwa walikaa na makundi hayo ili kujua ni changamoto gani wanazipata pale wanapo onana au kuwa na mgonjwa mwenye ugonjwa wa afya ya akili pia aliona kuwa kunahaja ya kuendelea kufanya utafiti huo wa awali.

Amesema kabla ya kutoa matokeo hayo waliweza kukutana na mzazi au Mlezi mmoja mmoja, mgonjwa mmoja mmoja ili kuangalia wanachokizungumza kinalingana ili kujua wanaanzia wapi katika kufanya utafiti huo kwa Mikoa ya nchi nzima.

"Wakati wa Utafiti tulichukua mtu, Mzazi, Mlezi au Muuguzi ambaye mgonjwa wa afya ya akili aliona na mtu wake wa msaada." Amesema Karina

Amesema katika utafiti huo wamegundua kuwa dawa inatibu lakini pia tiba kwa maongezi kwa wanafamilia inasaidia sana pale ambapo wanafamilia wanajua ugonjwa huo upo na wa aina gani na wajue kuwa ugonjwa upo kwaajili ya binadamu na binadamu yupo kwaajili ya magonjwa.

Akizungumza wakati wa kuwasilisha Matokeo ya awali ya Utafiti wa KUPAA, Profesa Sylvia Kaaya amesema kuwa chanzo cha Magonjwa ya afya ya akili ni kutengwa na jamii, Kuwa na Msongo, umasikini, uchawi, dawa za kulevya, kuwa na imani za kidini, kiwewe na mapepo.

Utafiti huo umebainisha njia 10 za kufikia unafuu kwa mtu aliyepatwa na magonjwa ya afya ya akili ni Kuwa na matumaini ya kuwa mgonjwa atapona, Msukumo binafsi, kumjumuisha mgonjwa kwenye familia, ushiriki wa kundi rika, uhusiano chanya, Utamaduni, kuzingatia matukio yanayoumiza, uwezo na uwajibikaji na kuthaminiwa.

Mkuu wa Idara ya maadili ya tafiti za Afya wa Taasisis ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (NIMR), Daktari Otilia Flavian amesema kuwa magonjwa ya afya ya akili waliyapa umuhimu katika sekta ya afya ili kutoa majibu kwa wakati ili afua zinazoenda kuwekwa zisichelewe kulingana matatizo yanayotokea katika jamii.

Amesema kuwa matokeo hayo ya awali wameyapokea lakini amewasa waandae mhutasari wa matokeo hayo na kuyawasilisha NIMR ili waweze kufikisha katika ngazi za maamuzi.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad