HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, June 15, 2022

UTOLEWAJI WA VYETI WARAHISISHWA KWA WOTE WANOENDA KUCHANJA CHANJO YA UVIKO 19

 Na Mwandishi Wetu

IKIWA imepita takribani miezi kumi (10) tangu chanjo za UVIKO 19 zianze kutolewa rasmi hapa nchini ambapo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan alitufungulia pazia hilo bado kama taifa hatujafikia malengo ya uchanjaji.

Lengo ambalo limewekwa na Shirika la Afya Duniani (WHO) ni kuwa ifikapo Disemba mwaka huu basi walau asilimia 70 ya watu wote duniani ambao wamekidhi vigezo vya kuchanja.

Kwa hapa nchini kumekuwa na sababu tofauti tofauti ambazo zinawafanya watu kuwa wazito kwenda kuchanja. Wapo ambao wana wasiwasi kuhusu utendaji kazi wa chanjo na wapo ambao sababu zao zimechangiwa na yale waliyoyasikia kwa wengine.

Amref Health Africa Tanzania wamekuwa mstari wa mbele kuhakikisha elimu inawafikia watu wote ili kujibu maswali yao na kuwaondolea wasiwasi ili waweze kuchukua hatua ya kwenda kuchanja.

Kupitia mahojiano mbali mbali ambayo Amref wamekuwa wakifanya na wataalam wa afya, elimu imeendelea kuwafikia watanzania wengi na hivyo kusaidia jitihada za serikali za kufikia malengo ya uchanjaji kitaifa.

Katika moja ya mahojiano hayo, walizungumza na Dkt. Devotha Protus anayesimamia kituo cha kutolea chanjo katika hospitali ya rufaa ya mkoa wa Dar Es Salaam (Mwananyamala) kuhusu utaratibu wa utoaji wa vyeti kwa wale ambao wamechanja chanjo ya UVIKO 19.

Kwa mujibu wa Dkt. Protus vyeti vya chanjo ya UVIKO 19 hutolewa kwa mtu pale tuu anapokuwa amekamilisha chanjo. Hii inamaana kwa wale wanaochanja chanjo ya mara moja hupatiwa vyeti mara tuu wamalizapo kuchoma chanjo na kwa wale wanaohitaji kuchoma chanjo zaidi ya mara moja hupatiwa vyeti pale tuu watakapokamilisha dozi.

Pia Dkt. Protus aliongeza kuwa hakuna ulazima wa mtu kufuata cheti kwenye kituo kile kile ambacho alipata chanjo yake ya kwanza. Ikiwa mtu huyu amefikisha muda wake wa kupata chanjo ya pili akiwa mbali ya kituo kile alichopatia chanjo ya kwanza anaweza kwenda kwenye kituo chochote kilicho karibu naye na kukamilisha dozi yake kisha kupatiwa cheti.

Bado jamii inakumbushwa kuendelea kuchanja na kujiweka salama na tayari endapo yakatokea mawimbi mapya ya ugonjwa huu hatari wa Korona.


 Dkt.Devotha Protus.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad