HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, June 3, 2022

TUZO ALIYOPATA RAIS SAMIA NI HESHIMA KWA TAIFA LETU

 

Mwenyekiti wa chama Cha wakandarasi Thobias Kyando akizungumza na waandishi wa habari kuhusu kongamano lililoandaliwa na wakandarasi wazawa kwa ajili ya kumpongeza Rais Samia.
Makamu Mwenyekiti wa ACCT Profesa mhandisi John Bulla  akizungumza na waandishi wa habari kuhusu kongamano lililoandaliwa na wakandarasi wazawa kwa ajili ya kumpongeza Rais Samia.
Mwanachama wa ACCT Mainda Waziri akizungumza na waandishi wa habari kuhusu kongamano lililoandaliwa na wakandarasi wazawa kwa ajili ya kumpongeza Rais Samia.

Na Mwandishi Wetu Dodoma
TUZO aliyoipata Mhe.Rais Samia Suluhu Hassan ni alama tosha kuwa amefanya vizuri Kimataifa katika ujenzi hasa wa miundombinu hivyo imewapa deni kubwa wakandarasi wazawa kuhakikisha kuwa wanaendelea kufanya kazi kwa ueledi na umakini mkubwa.

Tuzo hiyo ni heshima kubwa kwa taifa kwa ujumla huku ikitupa nafasi ya kupeleka pongezi zetu moja kwa moja kwa Rais kama wadau ambao ndio walengwa hasa wa tuzo hiyo.

Hayo yamezungumzwa leo jijini Dodoma na Mwenyekiti wa ACCT Thobias Kyando wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu kongamano lililoandaliwa na wakandarasi wazawa kwa ajili ya kumpongeza Rais Samia.

"Rais Samia amestahili kabisa kupewa tuzo hii ya heshima kwasababu amefanya mambo makubwa katika sekta ya miundombinu ikiwemo ujenzi wa reli ya kisasa, barabara, na bandari ndio maana akaibuka kidedea wa tuzo hiyo na sisi tukiwa wadau wa miundombinu tunampongeza sana,"amesema mwenykiti Kyando

Pia Ameeleza ujenzi wa miundombinu imekuwa na faida hasa kwa wandarasi Wazawa kwasababu wanahusika moja kwa moja kuiboresha pindi wakandarasi wageni wanapoondoka.

Mwenyekiti huyo ameiomba Serikali kuendelea kuwaamini wakandarasi wazawa kwa kuwapatia tenda mbalimbali ili waendelee kupata uzoefu hiyo itasaidia kuipunguzia serikali gharama ambazo imekuwa ikitumia kutoa tenda kwa kampuni za nje ya nchi.

"Ni vyema wakandarasi wazawa wakawa wanahusika moja kwa moja katika kutekeleza miradi mbalimbali inayotekelezwa hapa nchi hiyo itasaidia serikali kutumia fedha kidogo na kupata uzoefu kutoka kwa wakandarasi wa kigeni," amesema.

Naye amesema wamendaa kongamano kubwa litakalofanyika katika ukumbi wa Jakaya kikwete Dodoma lengo ni kutoa pongezi kwa Rais Samia kwa kutwaa tuzo ya heshima ambapo mgeni rasmi katika kongamano hilo ni Waziri wa ujenzi na uchukuzi Makame Mbarawa.

"Kesho ni pongezi kubwa kwa Rais wetu kwa kupata tuzo kubwa ambayo inatupa nguvu kwasababu hata sisi wakandarasi wazawa ameendelea kutujali kwa kutupatia kazi mbimbali za ujenzi tunachoomba tupewe fursa zaidi ili tuonyeshe uwezo zaidi kwasababu utaalamu unaweza ukanunuliwa kutoka nje kwa pale tutakapokwama,"amesema

Kwa upande wake Mwanachama wa ACCT, Maida Waziri amesema tuzo aliyoipata Rais Samia ni tuzo kubwa watanzania hawanq budi kuendelea kutambua na kuunga mkono jitihada mbalimbali zinazofanywa na serikali katika sekta ya miundombinu.

"Tuzo hiyo ameipata kutokana na ujenzi wa miundombinu kwa kweli tuna haki ya kujivunia sana kwa sababu kama watanzania Rais Samia ameleta tuzo hiyo kubwa napenda kusema kuwa watanzania tunaona dira na muelekeo wa serikali ya awamu ya sita tunaona njia kubwa huko tunakoenda," amesema.

Maida amesema kigezo cha nchi kuonekana ni tajili mara nyingi hupimwa kwenye ujenzi wa miundombinu na kwa tuzo hiyo ambayo Rais Samia ameipata ameonyesha watanzania kuwa Tanzania ni nchi tajiri.

"Rais Samia amepewa tuzo na Benki ya Afrika imetambua jitihada anazozifanya katika ujenzi wa miundombinu ya barabara ikiwemo miradi aliyoikuta iliyoanzishwa na hayati Dkt. John Magufuli na kuanzisha miradi mipya," ameeleza.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad