HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, June 8, 2022

TASAC Yawajengea uwezo Wahariri na Waandishi wa Habari

*Yaahidi kufanya kazi kwa ushirikiano na wadau kupata ufanisi wa utoaji wa huduma .

ZAIDI ya vyeti 4000 vya mabaharia hutengenezwa kwa Watanzania kutoka Shirika la Wakala wa Meli Tanzania(TASAC)

Shirika linadai kuwa kuna ajira nyingi ziko wazi katika usafirishaji kwa njia ya maji na kutaka watu kusoma fani mbalimbali zinazohusiana na na sekta na sekta ya usafiri majini.

Hayo ameyasema mwakilishi wa Mkurugenzi wa Uthibiti wa Usalama, Ulinzi wa vyombo vya Usafiri Majini na Utunzaji wa Mazingira wa majini (TASAC) baharia Gabriel Manase wakati wa mafunzo ya kuwajengea uwezo wahariri na waandishi wa habari iliyofanyika mjini Bagamoyo mkoani Pwani.

Katika mafunzo hayo Baharia Manase amesema mafanikio hayo ya utoaji wa vyeti ni fursa ya ajira kwa wanzania ndani na nje ya nchi. Mafanikio hayo yamepatikana katika kipindi kifupi cha mwaka wa fedha 2021/2022.

Aidha amesema kumekuwa na hitaji kubwa la mabaharia katika meli za kimataifa hivyo kuwepo na uhitaji wa vijana kufanya kazi hiyo na hivyo kusisitiza zaidi wajitokeze kusoma fani hiyo yenye ajira nyingi Duniani.

Amesema kuna kampuni inataka mabaharia 400 lakini katika soko la Tanzania ni fursa kwani kwa uhitaji huo ni vyema vijana kufanya maamuzi ya kusoma fani hizo.
Mmoja ya wahariri akiuliza swali wakati wa kuwajengea uwezo Wahariri na Waandishi Habari Bagamoyo Mkoani Pwani leo Juni 8, 2022.
Mkurugenzi wa Huduma za Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC), Moses Rajab Mabamba akizungumza wakati wa kuwajengea uwezo Wahariri na Waandishi Habari Bagamoyo Mkoani Pwani leo Juni 8, 2022.
Mwakilishi wa Mkurugenzi wa Uthibiti wa Usalama, Ulinzi wa vyombo vya Usafiri Majini na Utunzaji wa Mazingira wa majini (TASAC) baharia Gabriel Manase akizungumza wakati wa kuwajengea uwezo Wahariri na Waandishi Habari Bagamoyo Mkoani Pwani leo Juni 8, 2022.
Ofisa Sheria TASAC, Vedastus Kitureti akizungumza wakati wa kuwajengea uwezo Wahariri na Waandishi Habari Bagamoyo Mkoani Pwani leo Juni 8, 2022.











Baadhi ya Wahariri na Waandishi Habari wakijengewa uwezo na TASAC Bagamoyo Mkoani Pwani leo Juni 8, 2022.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad