Na Mwandishi Wetu, Bukoba
Waendesha
pikipiki maarufu kama bodaboda mkoani Kagera wamempongeza Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan kwa kupunguza
gharama za mafuta.
Hatua ya kupunguza bei ya mafuta ilitokana na
mtazamo chanya wa serikali wa kubana matumizi na kutoa ruzuku ya
shilingi bilioni 100, jambo ambalo limesaidia kushuka kwa bei hapa
nchini na kupunguza makali ya maisha.
Pongezi za bodaboda hao
zimewasilishwa na Umoja wa Bodaboda wilayani Bukoba (UBOBU) ikiwa ni
siku moja kabla ya Rais Samia kufika mkoani Kagera kwa ajili ya ziara ya
kikazi ya siku tatu mkoani humo.
Mwenyekiti wa UBOBU, Mahamud
Sued amesema ushushaji wa bei ya mafuta utalisaidia kundi kubwa la
bodaboda kuweza kumudu gharama za maisha na kuepuka kujiingiza kwenye
vitendo viovu.
"Ili kutambua ukubwa wa kundi hili kwa upande wa
Manispaa ya Bukoba pekee kuna bodaboda 8,600 ndio maana tunaomba
aendelee kutupunguzia gharama.
Ruzuku imetolewa kwa wakati muafaka na kutupa nahueni sisi ambao riziki zetu zinategemea sana bei ya mafuta."
Kabla
ya kutolewa kwa ruzuku hiyo, kwa Bukoba mafuta yalikuwa yanauzwa
shilingi 3,460 kwa Lita na Sasa yanauzwa shilingi 3,200 kwa lita kukiwa
na punguzo ya shilingi 260 kwa lita.
"Pia bodaboda tunamuomba
Rais Samia kurasimisha biashara ya bodaboda na kulitambua kama kundi
maalum lenye uhitaji wa kuwekewa mazingira mazuri ya kibiashara kama
inavyofanyika kwa wamachinga.
Kundi hili tupo watu wa kila aina,
kuanzia waliomaliza darasa la saba au chini zaidi mpaka waliomaliza vyuo
vikuu lakini wakakosa ajira. Wote tumejiingiza humu na kujiajiri
kutafuta kipato ili kulea familia na wategemezi wetu kwa kufanya kazi
halali ya uendeshaji wa bodaboda," alisema Sued.
Naye Naibu
Waziri wa Nishati, Adv Steven Byabato alisema katika suala la kutoa
ruzuku hiyo, Rais Samia ameupiga mwingi tena wa kimataifa kwa sababu
mafuta hayajashuka bei bali Rais Samia ameshusha bei ya mafuta kwa
kuweka hiyo fedha ya ruzuku.
Alisema kinachotakiwa ni kumuombea
ili Rais Samia aweze kupambana kutafuta namna ya kushusha zaidi bei hiyo
kwa kutafuta fedha nyingine zitakazosaidia punguza gharama kwa
wananchi.
"Kwa sababu isingeweka hiyo ruzuku sasa hivi Bukoba tungekuwa tunanunua mafuta 3700 au 3800 pengine hata na zaidi.
Na
bei hiyo inaendelea kupanda duniani kwa sababu upatikanaji wa bidhaa
hiyo ni mdogo kuliko uhitaji wake ambao ni mkubwa," alisema Byabato.
Byabato
alisema kwa Tanzania mafuta hayashuka bali kutokana na huruma ya Rais
inayotokana na umama ameamua kuweka fedha hizo ili kushusha bei kwa
lengo la kupunguza ukali wa maisha.
"Katika kitu ambacho Rais
Samia ametusaidia ni kuweka shilingi bilioni 100, na ninawaahidi huko
tunakoelekea ni kuzuri zaidi," alisisitiza.
Wednesday, June 8, 2022

BODA BODA BUKOBA WAMPONGEZA RAIS SAMIA,WAOMBA WARASIMISHWE
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment