Tumeendelea
kupokea na kufuatilia mwenendo wa taarifa za uwepo wa TEMBO katika
maeneo ya kata za Mkiwa na Misughaa wilaya ya Ikungi
Ofisi
ya mkuu wa wilaya kwa kushirikiana na mamlaka zingine wanaendelea
kuwafuatilia Tembo wanaonekana katika makazi ya watu katika maeneo tajwa
Aidha
ofisi ya wilaya kwa kushirikiana na mamlaka zingine imefanya kikao kazi
na Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt. Binilith S. Mahenge Jana Tarehe
20/06/2022 na kukubaliana kuchukua hatua zaidi za kudhibiti Tembo
walioko kwenye makazi ya wananchi
Kwa
Taarifa hii, tunaomba wananchi katika maeneo tajwa kuendelea kuchukua
tahadhari ya usalama wao, pia tunaomba wananchi kuacha Tabia ya
kuwashambulia, kuwakimbiza au kuwasongasonga Tembo wanaopita katika
maeneo yao badala yake watoe taarifa kwa mamlaka husika za vitongoji,
vijiji, kata na hata wilaya
Ofisi
ya Mkuu wa wilaya Ikungi inapenda kuwahakikisha wananchi Serikali
inafanya kila linalowezekana katika mamlaka zetu kuondoa changamoto kwa
haraka.
Imetolewa na ofisi ya Mkuu wa Wilaya Ikungi
21/06/2022
No comments:
Post a Comment