HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, June 29, 2022

Rais Samia Mgeni Rasmi Siku ya Kiswahili Duniani

 Na Shamimu Nyaki

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kuwa Mgeni Rasmi katika Maadhimisho ya Siku ya Kiswahili Duniani yatakayofanyika kitaifa Julai 07, 2022 jijini Dar es Salaam

Akizungumza na waandishi wa habari leo Juni 29, 2022 , Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Amos Makalla, amesema kuwa, analishukuru Shirika la UNESCO nchini kwa kuendelea kuipa heshima lugha ya Kiswahili kwa kuadhimisha siku hiyo maalumu kila Julai 7

"Maadhimisho haya kwa mwaka huu ni ya kipekee sana , tunatarajia kupata wageni wengi mashuhuri kutoka ndani na nje ya nchi, akiwemo Rais Mstaafu wa Msumbiji Mhe.Joachim Chisano, Rais Mstaafu wa Namibia Mhe. Sam Nujoma, hii ni heshima kubwa kwa mkoa wetu " alisema Mhe. Makalla.

Ameongeza kwa kueleza kuwa, maadhimsho hayo yatahusisha shughuri mbalimbali ikiwemo kongamano kuhusu mchango wa lugha ya Kiswahili katika Harakati za Ukombozi wa Bara la Afrika, litakalofanyika Julai 06, 2022 ambapo Balozi Mstaafu Mhe. Ame Mpungwe ataongoza mada mbalimbali.
Maadhimisho hayo yatatanguliwa na Tamasha la Utamaduni la Kwanza Kitaifa ambalo litafanyika katika Uwanja wa Uhuru kuanzia Julai 01 hadi 03, 2022.Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Amos Makalla Akizungumza na Waandishi wa Habari jijini hapo leo Juni 29, 2022 kuhusu Tamasha la Utamaduni la Kwanza Kitaifa litakalofanyika kuanzia Julai 01 hadi 03, 2022 katika Uwanja wa Uhuru na kuelekea kilelele cha maadhimisho ya Siku ya Kiswahili Duniani Julai 07, 2022.Kushoto ni Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo Bw. Saidi Yakubu

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad