HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, June 13, 2022

Mbunge ajitosa suala la utoaji mimba usio salama unavyoota mizizi nchini Tanzania

 

SUALA la utoaji mimba usio salama limekuwa gumzo katika siku za hivi karibuni na takwimu zinaonyesha vifo vitokanavyo na uzazi husababishwa na sababu mbalimbali ikiwemo utoaji mimba usio salama.

Sote tunafahamu kwamba kwa hapa Tanzania suala la utoaji wa mimba haliruhusiwi kisheria, japo Wizara ya Afya imefanya jitihada mbalimbali ikiwemo kutoa miongozo ya baada ya mimba kuharibika,(Comprehensive Post Abortion Care CPAC)ili kuwaongoza watoa huduma za afya waweze kutoa huduma pale tu mwanamke akifanyiwa ukatili wa kijinsia kama ubakaji au baba au mtu wakaribu kumpa mimba mtoto wake wa kumzaa au ndugu wakaribu.

Licha ya sheria kukataza utoaji mimba,vitendo hivyo hufanyika na mara nyingi kwa njia zisizo salama pamaja na kwamba takwimu zinaonesha kwamba tatizo la vifo vya uzazi linapungua,bado kuna baadhi ya mambo yanachangia kuwepo ikiwemo suala la utoaji mimba usio salama.

Wataalamu wanasema huduma hii ni muhimu sana kwa waathirika kwa sababu hutolewa kwa ajili ya kulinda usalama wa afya ya waathirika wa tukio na huduma hiyo mwanamke anatakiwa kuzipata ndani ya muda mfupi tangu kuharibika kwa mimba ikiwepo kusafisha kizazi pamoja na kupewa dawa maalumu.

Takwimu zinaonyesha katika kila Wanawake100,000 kunatokea vifo 454 mpaka vifo 556(Taarifa kutoka 2015/2016 TDHS) vifo hivi visababishwavyo na utoaji wa mimba usio salama vinaonesha kuwa katika 16% mpaka 30%.

Hivi karibuni Mbunge wa Viti maalumu ,Judith Kapinga aliongelea suala la utoaji mimba usio salama na kutoa baadhi ya takwimu na kuomba Waziri wa Afya kutoa muongozo kuhusu suala hilo bungeni,Mei 30,2022.

Mbunge huyo alieleza kwa kina jinsi tunavyopoteza nguvu kazi nyingi kutokana na vifo vya wanawake vitokanavyo na utoaji mimba usio salama na hivyo kumwomba Waziri kutengeneza utaratibu ili huduma hiyo iweze kupatikana kwa utaratibu mzuri na salama.

“Mwanamke anatumika kama nyenzo bora katika suala la maendeleo ninachosikitika suala la utoaji wa mimba mitaani limeachiwa kupita maelezo”Mbunge Judith Kapinga

Anasema twakwimu zinaonesha kwa wanawake laki 400,000 kila mwaka wanatoa mimmba mitaani na asilimia 70% wanatumia yenzo ambazo siyo za madakatari wenye sifa huku ni asilimia 30% tu wanawake wa mijiini ambao wataenda kwa madktari wenye sifa.

“Masuala ya utoaji haya ya mimba inawezekana tusiyaongee sana wanawake 400,000 kwa mwaka ni saw ana wanawake 1100 kila siku wanatoa mimba kwa njia zisizo salama Mheshimiwa Waziri tunaomba ulifanyie kazi hilo suala”anasema Mbunge Judith Kapinga

Nafahamu kwamba kuna namna ambavyo mwanamke anaruhusiwa mimba hivyo kuna mambo ambayo tunaweza kuyaboresha iliwanawake wasikimbilie mitaani kwenye nyenzo zisizo salama ili waende katika mahala salama katika suala hilo.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad