HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, June 13, 2022

DK. GWAJIMA ATETA NA UNESCO JUU YA KUKABILIANA NA UKATILI WA KIJINSIA KWA WANAWAKE NA WATOTO

 

Na Mwandishi wetu
WAZIRI wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maaalumu, Dk Dorothy Gwajima ameliomba Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) kutumia miundo mbinu yake iliyopo nchini kukabiliana na ukatili wa kijinsia kwa wanawake na watoto.

Dk. Gwajima alitoa ombi hilo wakati wa kikao chake na Kaimu Mwakilishi Mkazi wa Shirika hilo, Faith Shayo na ujumbe wake katika ukumbi wa Chuo cha Ustawi wa Jamii jijini Dar es Salaam.

Alisema Unesco imesaidia sana serikali katika kukabiliana na ukatili wa kijinsia kupitia mkakati wa kitaifa ulizinduliwa mwaka 2017 na kumalizika Juni mwaka huu.

Alifafanua kwamba kupitia mkakati huo Unesco imefanya kazi kubwa na kwamba wanaitarajia kushiriki pia katika mkakati ujao wa miaka mitano wenye lengo kupaza sauti kupinga ukatili.

“Wakati tu najiandaa kwa siku ya mtoto wa Afrika na mkakati mpya wakati taifa linajiandaa kuanza mkakati mpya hali ya sasa inahitaji ushirikiano wa dhati wa wadau wote ili kurejesha usalama kwa wanawake na watoto,” alisema.

Dk Gwajima alisema ukatili kwenye hali ya ulawiti na ubakaji umezidi hivyo inahitaji jamii nzima kupaza sauti kupinga hali hiyo huku akiwataka wanaume wenye nia njema kuunda jukwaa la kukemea matendo yanayotokea sasa wanayobebeshwa na wanaume mabazazi wachache.

Alisema anatambua kwamba UNESCO ina miundombinu ya kutosha hasa radio ambazo zinawafikia wananchi kwa kulingana na maeneo na kwamba serikali ingelipenda kutumia mfumo ya kupasha habari ya UNESCO kuendesha kampeni kubwa ya kupinga ukatili.

Hivi karibuni taarifa za ubakaji, unajisi watoto pamoja na vipigo na mauaji kwa dai la wivu wa mapenzi vimeongezeka sana nchini kiasi cha kufanya Bunge la 12 katika mkutano wake wa saba kuendesha mjadala wa kutosha kuhusiana na kadhia hiyo.

Akizungumza katika kikao hicho Kaimu Mwakilishi Mkazi wa Shirika hilo, Faith Shayo alisema kwamba UNESCO ipo tayari kushirikiana na serikali kuinua ustawi wa jamii kupitia kuboreka kwa mahusiano ya kijinsia na kuondoa ukatili.

Pamoja na kutoa ahadi ya kushirikiana na serikali pia ameipongeza kampeni ya mlango kwa mlango iliyoanzishwa na wizara ya kukabiliana na ukatili wa kijinsia dhidi ya wanawake na watoto.

Alisema ingawa UNESCO inaendelea kushirikiana na serikali katika kutoa elimu ya afya na huduma za jamii kupitia miradi yake inayofadhiliwa na O3 Plus na UN Joint Programme on AIDS (UBRAF) katika vyuo nchini Tanzania na nchi za Jumuiya ya SADC ili kutengeneza makazi salama, UNESCO ipo tayari kuingia makubaliano na serikali juu ya namna bora ya kukabilina ana ukatili wa kijinsia.

Alitaja baadhi ya miradi ambayo UNESCO inaendelea kushirikiana na serikali ni pamoja na kuwawezesha wafanyakazi na viongozi kuhusu ukatili wa kijhinsia unavyokuwa na namna ya kukabiliana nao na kuwezesha kuwapo kwa kozi zinazozungumzia ukatili wa kijinsia.

Aidha alisema kwa siku za karibuni UNESCO ilitiliana saini na vyuo vikuu vya UDSM, UDOM, MUCE na DUCE vya kuendesha mradi wa kukabiliana na ukatili wa kijinsia vyuoni wenye gharama ya Sh 92,368,400.00

Naye Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Habari UNESCO, Nancy Kaizilege alisema kwamba mifumo ya redio inayosaidiwa na UNESCO ipo tayari kusaidiana na serikali katika kampeni yake na kumtaarifu Waziri Dk Gwajima kwamba anapoenda ziara anaweza kuzitumia redio hizo.

Alisema kwamba kwa sasa hali ya ukatili si nzuri na lazima jamii ifanye kitu ili kuzuia hali isiwe mbaya na kurejesha usalama kwa wanawake na watoto

Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wanawake na Makundi Maaalum, Dkt. Dorothy Gwajima akizungumza na Kaimu Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO), Faith Shayo (kulia) na ujumbe wake wakati wa kikao cha kuboresha ushirikiano kuelekea maandalizi ya kampeni ya kitaifa ya kupinga ukatili wa kijinsia kilichofanyika katika ukumbi wa Chuo cha Ustawi wa Jamii jijini Dar es Salaam. Wengine ni Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Habari UNESCO, Nancy Kaizilege( wa pili kulia),Msaidizi wa Mwakilishi Mkazi wa UNESCO, Roseline Muhangachi (wa tatu kulia) Afisa Utawala wa ofisi za UNESCO, Adankegn Mekonnen (wa nne kushoto), Ofisa wa Kitaifa anayeshughulikia Elimu ya Afya na Ustawi wa ofisi za Unesco Dar es Salaam, Mathias Herman (wa tatu kushoto) pamoja na Mkurugenzi wa Maendeleo ya Watoto wa Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Watoto, Ndg Sebastian Kitiku (wa pili kushoto).
Kaimu Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO), Faith Shayo (kulia) akifafanua jambo kwa Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wanawake na Makundi Maaalum, Dkt. Dorothy Gwajima (hayupo pichani) wakati wa kikao cha kuboresha ushirikiano kuelekea maandalizi ya kampeni ya kitaifa ya kupinga ukatili wa kijinsia kilichofanyika katika ukumbi wa Chuo cha Ustawi wa Jamii jijini Dar es Salaam. Wa pili kulia ni Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Habari UNESCO, Nancy Kaizilege pamoja na Msaidizi wa Mwakilishi Mkazi wa UNESCO, Roseline Muhangachi.
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Habari UNESCO, Nancy Kaizilege (katikati) akisisitiza jambo kwa Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wanawake na Makundi Maaalum, Dkt. Dorothy Gwajima (hayupo pichani) wakati wa kikao cha kuboresha ushirikiano kuelekea maandalizi ya kampeni ya kitaifa ya kupinga ukatili wa kijinsia kilichofanyika katika ukumbi wa Chuo cha Ustawi wa Jamii jijini Dar es Salaam. Kulia ni Kaimu Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO), Faith Shayo pamoja na Msaidizi wa Mwakilishi Mkazi wa UNESCO, Roseline Muhangachi.
Ofisa wa Kitaifa anayeshughulikia Elimu ya Afya na Ustawi wa ofisi za Unesco Dar es Salaam, Mathias Herman (katikati) akizungumza na Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wanawake na Makundi Maaalum, Dkt. Dorothy Gwajima (hayupo pichani) wakati wa kikao cha kuboresha ushirikiano kuelekea maandalizi ya kampeni ya kitaifa ya kupinga ukatili wa kijinsia kilichofanyika katika ukumbi wa Chuo cha Ustawi wa Jamii jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Mkurugenzi wa Maendeleo ya Watoto wa Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Watoto, Ndg Sebastian Kitiku na Kulia ni Afisa Utawala wa ofisi za UNESCO, Adankegn Mekonnen.
Kaimu Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO), Faith Shayo (kushoto) akimkabidhi Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wanawake na Makundi Maaalum, Dk. Dorothy Gwajima makabrasha ya Shirika la UNESCO mara baada ya kumaliza kikao cha kuboresha ushirikiano kuelekea maandalizi ya kampeni ya kitaifa ya kupinga ukatili wa kijinsia kilichofanyika katika ukumbi wa Chuo cha Ustawi wa Jamii jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wanawake na Makundi Maaalum, Dk. Dorothy Gwajima katika picha ya pamoja na Kaimu Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO), Faith Shayo na ujumbe wake mara baada ya kumaliza kikao cha kuboresha ushirikiano kuelekea maandalizi ya kampeni ya kitaifa ya kupinga ukatili wa kijinsia kilichofanyika katika ukumbi wa Chuo cha Ustawi wa Jamii jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wanawake na Makundi Maaalum, Dk. Dorothy Gwajima katika picha ya kumbukumbu na Kaimu Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO), Faith Shayo mara baada ya kumaliza kikao cha kuboresha ushirikiano kuelekea maandalizi ya kampeni ya kitaifa ya kupinga ukatili wa kijinsia kilichofanyika katika ukumbi wa Chuo cha Ustawi wa Jamii jijini Dar es Salaam.


No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad