UBALOZI wa Ufaransa nchini kwa kushirikiana na
WePresent Tanzania wameandaa tamasha Hip Hop asili kwa msimu wa pili
litakalofanyika kwa siku tatu za Juni 23 hadi 25 kuanzia saa tano
asubuhi hadi saa sita usiku katika ukumbi wa Alliance Francaise jjini
Dar es Salaam kwa kiingilio cha shilingi 10,000 kwa siku na shilingi
20,000 kwa siku tatu za tamasha hilo.
Akizungumza
na waandishi wa habari wakati kuzindua msimu wa pili wa tamasha hilo
Balozi wa Ufaransa nchini Tanzania Nabil Hajlaoui amesema kuwa, tamasha
hilo litawaweka vijana pamoja na kuwakilisha mawazo yao kupitia sanaa
pamoja na kujitangaza.
''Tanzania,
nchi za Afrika Mashariki, Marekani na Ufaransa watashiriki tamasha hili na kuleta
thamani juu ya sanaa ambayo hudhaniwa ni kwa ajili ya kundi la wanaume
pekee au kwa ajili ya kundi fulani, tutashuhuda sanaa za deejaying, MC's
tutegemee burudani kwa siku tatu za tamasha hili.'' Amesema Balozi
Nabil.
Aidha
amesema kuwa tamasha hilo limeungwa mkono na ubalozi wa Ufaransa
Tanzania, Alliance Francaise Dar es Salaam pamoja na ubalozi wa Marekani
Tanzania na ni mwendelezo wa tamasha lililofanywa na wana Hip Hop 30 wa
Afika na Ufaransa Oktoba mwaka jana katika mkutano wa New Africa-Fance
Summit (NSAF,) ambao ulichochea kuandaliwa kwa mkakati wa ushiriki wa
Hip Hop kwa bara la Afrika kwa mwaka 2022/2024.
Kwa
upande wake Mkurugenzi wa kituo cha utamaduni cha Alliance Francaise
Frola Valleur amesema kuwa, tamasha hilo limelenga kujenga ushirikiano
pamoja na kutangaza sanaa na tamaduni za Tanzania na Afrika Mashariki
kwa ujumla ulimwenguni.
Amesema
tamasha hilo la siku tatu limeandaliwa mahususi katika kusherekea
utamaduni wa Hip Hop Afrika Mashariki na litaambatana na sanaa nyingine
nyingi ikiwemo breakdancng, emceeing, graffiti, deejaying, beeat boxing
pamoja na boarding.
''Siku ya tarehe 24
Juni kutakuwa na shindano la break dance la Afika Mashariki na kupata
bingwa wa Tanzania ambaye atawakilisha kwenye 'Battle of the Year 2022
' nchini Japan, siku ya tarehe 25 tamasha litapambwa na wasanii
Octopizo kutoka Kenya, Tina Mweni wa Kenya/ Denmark, Rise up Band ya
Tanzania/ Ufaransa, Jay Moe wa Tanzania, The Mc 255 wa Tanzania, Mic
Crenshaw wa Marekani, Lord Eyes wa Tanzania pamoja na wengine wengi
watapamba tamasha hili.'' Amesema.
Aidha
amesema, warsha hiyo ya siku tatu litabeba maudhui mbalimbali ikiwemo
historia ya Hip Hop Tanzania, sanaa ya emcee, breakdance, beat box
kupitia wawezeshaji Bboy Lilou kutoka Ufaransa ambaye pia ni bingwa wa
dunia wa breakdance pamoja na Deejay PH wa Ufaransa, Mejah Mbuya wa
Tanzana pamoja na Mama C wa Tanzania/ Marekani.
Amesema
kituo hicho cha utamaduni kilianzishwa mwaka 1961 nchini kwa malengo
ya kufundisha lugha ya Kifaransa ambapo mwamko wa watanzania ni mkubwa
pamoja na kueneza utamaduni wa Tanzania ulimwenguni.
''Tanzania
ina mwamko mkubwa wa kujifunza Kifaransa hadi sasa tuna wanafunzi
wapatao 450 na katika kueneza utamaduni wa Tanzania katika msimu huu wa
tamasha la pili na HipHop asili wasanii kutoka nchi za Kenya, Uganda,
Rwanda, Burundi, Kongo, Ghana, Ufaransa na Marekani wataungana
na wanamuziki 36 waliochaguliwa kupitia mashindano ya Hip Hop asili
kutoka mikoa sita ya Tanzania ikiwemo Mwanza, Mbeya, Dar es Salaam,
Dodoma, Mwanza, Arusha, Dar es Salaam na Zanzibar.'' Amesema.
Kwa
upande wake mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi wa Alliance Francaise
Mkuki Byoga ameeleza kuwa kwa miaka 20 sasa sanaa imekuwa kwa kasi
ikiwemo muziki wa Bongo Flavour ambao umekua kupitia sanaa ya Hip Hop na
kuchangia katika pato la taifa na kupitia jukwaa hilo itaiweka Hip Hop
hai zaidi na kwa nchi za Afrika ambazo pia zinashiriki katika tamasha
hilo na duniani kwa ujumla.
.jpeg)

Muongozaji
wa tamasha hilo Mathieu Bruno (kushoto,) akizungumza na waandishi wa
habari wakati wa hafla hiyo na kueleza kuwa wamejipanga na wanatumaini
kupata matokeo chanya ya tamasha hilo kwa mwaka 2022.
Mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi wa Alliance Francaise
Mkuki Byoga (katikati,) akizungumza wakati wa hafla hiyo na kueleza kuwa kwa miaka 20 sasa sanaa imekua kwa kasi
ikiwemo muziki wa Bongo Flavour ambayo imekua kupitia kupitia sanaa ya Hip Hop na kuchangia
katika pato la taifa kwa kiasi kikubwa. Leo jijini Dar es Salaam.
Matukio mbalimbali wakati wa hafla hiyo.
No comments:
Post a Comment