Na Mwamvua Mwinyi, Kibaha
KIONGIZI
wa mbio za Mwenge Kitaifa Sahir Geraruma, amekemea baadhi ya watendaji
na viongozi wanaopuuzia mambo kwenye miradi ya maendeleo kwani kwa
kufanya hivyo ,ni kusababisha kuchelewa kwa miradi na kuwaacha wananchi
wakiendelea kutaabika.
Pia ameendelea kusisitiza uhifadhi wa nyaraka za miradi kwa Ajili ya kumbukumbu za ukaguzi .
Akiweka
jiwe la msingi Mradi wa Kituo cha Afya Pangani, Mji wa Kibaha Mkoani
Pwani ,Geraruma, aliwaasa baadhi ya viongozi na watendaji waache kufanya
kazi kwa mazoea kwa maslahi ya wananchi.
Akipokea
taarifa ya dawa za kulevya -kata ya Mwendapole, Geraruma aliwaasa
vijana kuacha kujiingiza katika matumizi ya dawa za kulevya kwani
zinamaliza nguvu kazi ya kundi la vijana.
Aliwataka
wachapekazi na kujiingiza katika vikundi mbalimbali vya ujasiliamali
kujishughulisha kuliko kupoteza muda kuvuta bangi, ama kutumia madawa ya
kulevya ambayo yanaathari kwao kiafya .
Geraruma
alitoa Rai kwa wale walio tayari kuacha madawa ya kulevya waache na
waanze dawa zitakazowasaidia kuacha kwa kuondoa makali ya wingi wa dawa
hizo mwilini (methadone).
Awali
akipokea mbio za Mwenge wa Uhuru Halmashauri ya Mji wa Kibaha ukitokea
wilaya ya Kisarawe , kwenye viwanja vya stendi ya zamani Mailmoja, Mkuu
wa wilaya ya Kibaha ,Sara Msafiri alisema mwenge huo utatembelea miradi
11 yenye thamani ya sh.Bilioni 1.6.
Alieleza
kwamba, kati ya miradi hiyo mradi mmoja utazinduliwa ,miwili itawekwa
jiwe la msingi ,miwili itatembelewa ,sita ujumbe wa mwenge itapokelewa
na mmoja ambao Ni wa Kukabidhi vifaa vya ujenzi Shule ya Sekondari Sofu,
huku ukikimbizwa kwenye umbali wa Km. 68.7.
Miradi
hiyo iliyotembelewa na kukaguliwa Ni Pamoja na Mradi wa malaria Kituo
cha Afya Mkoani,Ujenzi wa madarasa Shule ya Sekondari Bundikani, na
Mapambano dhidi ya rushwa - Shule ya Sekondari Bundikani.
Miradi
mingine ,Ni barabara ya lami Picha ya Ndege - Lulanzi, Kutembelea
kiwanda cha Mtanga Polytechnic - Sofu, Kupokea taarifa za lishe, VVU,
Sensa ya Watu na Makazi - viwanja vya Kwa Mbonde,kata ya Picha ya
Ndege,Kutembelea Kikundi cha Vijana cha Republic kilichopo Mwendapole.
No comments:
Post a Comment