HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, May 17, 2022

RPC LUTUMO AKEMEA WIZI WA NG'OMBE MKOANI PWANI

 
Kamanda wa polisi Mkoani Pwani, (ACP) Pius Lutumo

Na Mwamvua Mwinyi, Pwani
JESHI la polisi Mkoani Pwani, limekamata Watuhumiwa 54 kwa makosa mbalimbali yakiwemo ya wizi wa mifugo aina ya ng'ombe.

Kamanda wa polisi Mkoani Pwani, (ACP) Pius Lutumo alisema Jeshi hilo ,aliwataka wafugaji Kuwa na tahadhali kwa kuimarisha ulinzi na kuweka alama kwenye mifugo yao ili kupunguza wizi wa mifugo , ikiwa jeshi nalo linaendelea kulinda raia na Mali zao wakiwemo wafugaji.

Alieleza wamekamata ng'ombe 13 ambapo mtuhumiwa mmoja akiwa na ng'ombe sita amekamatwa anawasafirisha toka Chalinze kwenda Dar kwa kutumia gari namba T.125 BML Toyota canter.

Vilevile Watuhumiwa watatu wakiwa na ng'ombe saba wa wizi , pikipiki nne za wizi ,gari aina ya Toyota canter yenye namba za usajili T.125 BML , Televisheni tatu nch 32, monitor mbili,CPU ,vifaa vya magari ikiwa Ni Pamoja na taa kumi,side mirror moja na speed meter.

Lutumo alitaja, vifaa vingine ni pump tatu za kuvutia maji na mashine yake moja, external driver na laptop sita.

"Bangi Puli 65 na kete 521,gongo madumu sita,ndoo ndogo tatu zikiwa na lita 183 na mitambo miwili ya kutengeneza gongo.!"

Watuhumiwa watafikishwa mahakamani baada ya upelelezi kukamilika na kusema jeshi Hilo limejipanga kupambana na makosa ya wizi wa mifugo na uhalifu mbalimbali.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad