HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, May 17, 2022

MKOA WA KIPOLISI RUFIJI WAKAMATA WATUHUMIWA 59 WA MAKOSA MBALIMBALI-ACP MALULU

 

Na Mwamvua Mwinyi,Rufiji
KAMANDA wa Polisi,Mkoa wa Kipolisi Rufiji, Kamishna Msaidizi (ACP) Kungu Malulu amesema wataendelea kushughulika na wauzaji na watumiaji madawa ya kulevya aina ya bangi na wezi wanaovunja nyumba za watu kuiba vitu mbalimbali vya ndani.

Akitoa taarifa ya msako walioufanya wiki moja ,alisema wamekamata watuhumiwa 59 ,pamoja na vifaa vya kuvunjia milango kama nyundo, bangi ndoo kumi, ving’amuzi 2,televisheni, laptop 3 , radio subwoofer 7 na, magodoro matatu.

Malulu alieleza, Watuhumiwa hao Ni wa matukio hayo yakiwemo ya uvunjaji, ubakaji,nyara za Serikali, wizi wa mifugo na uuzaji/utumiaji madawa ya kulevya .

'"Tumekamata lita 147 za pombe aina ya gongo, Wilaya ya Rufiji pikipiki moja isiyokuwa na namba za usajili aina ya Sanlg, kupatikana na mali za wizi na Kutumika katika uhalifu. "

"Kati ya pikipiki saba zilizokamatwa Wilaya ya Mkuranga pikipiki nne’
MC965 CZJ aina ya TVS rangi nyeusi, MC610 DFX aina ya hunter rangi nyeusi,
nyeusi, Wilaya ya Kibiti pikipiki 1 MC957 DBMaina ya TVS rangi nyeusi,
tindo 2, plaizi 1 na bisibisi 3. "

Alisema pia wamekamata TV 8 ,
lock za madirisha ya vioo na kifaa cha kukatia nyavu za madirisha, vielelezo vilikamatwa ikiwa ni kwa ajili ya kuvunjia na kung’olea lock za milango,
MC258 CXRaina ya haojue rangi nyeusi na MC946 CUXaina ya boxer rangi
ya Mafia pikipiki 1 MC365 BK aina ya TVS.

Malulu alieleza ,hali ya mkoa wa Kipolisi Rufiji ni shwari, wananchi wanaendelea na shughuli zao halali za maendeleo pasipo hofu yoyote.

Kwa upande wa usalama barabarani kwa kipindi cha kuanzia Mei 9 mwaka huu, wamekamata magari yapatayo 465 sawa na sh.milioni 15.5 ,jumla ya magari yaliyokaguliwa 2,550 ambapo yaliandikiwa.

Makosa 1058 kati ya makosa 952 ni makosa yanayohusisha magari na 106 ni makosa ya jinai na uhalifu mbalimbali.

Kamanda wa Polisi mkoa wa Kipolisi anawashukuru na anawasihi wananchi
Kuendelea kushirikiana na jeshi la polisi.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad