HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Saturday, May 21, 2022

MTWARA KWELI KUCHELEEEE YATOA MISS TANZANIA

 Na.Khadija Seif, Michuzitv

MSHINDI wa Miss Tanzania mwaka 2022 aeleza namna alivosota kulisaka taji hilo kwa misimu miwili mfululizo katika Mashindano hayo.

Akizungumza mara baada ya kukabidhiwa zawadi yake ya gari aina ya Mercedes Benz class c200 katika usiku wa kuamkia mei 21 jijini Dar es salaam Halima Kopwe anaewakilisha kanda ya Mashariki Mkoa wa Mtwara amesema hii sio mara ya kwanza kwake kushiriki Shindano hilo.

"Nimeshashiriki 2018,2019 lakini sikukata tamaa nikaamua nitupe tena karata yangu katika Mashindano haya hatimae leo rasmi nimepewa dhamana na Watanzania na kuanzia leo nasimama kama muwakilishi wa Mashindano ya dunia (Miss world)."

Hata hivyo Kopwe amesema kiasi cha shilingi Milioni 10 alichopewa mbali na zawadi ya gari ataweza kuweka Fedha kidogo Kwa ajili ya Maandalizi rasmi ya kushiriki Miss world.

Hata hivyo Miss Tanzania 2020 Rose Manfere ambae amevua taji hilo rasmi Kwa Sasa amesema anashukuru watanzania wote Kwa kumpa ushirikiano wa kutosha hivyo anategemea Mrembo huyo mpya Halima ataendelea na Mazuri mengi zaidi Ili kuendelea kuonyesha hekima na nidhamu katika Sekta hiyo ya urembo .

Aidha katika Fainali hiyo Mshindi wa pili aliibuka Angel Mtatiro akikabidhiwa hundi ya shilingi milioni 5,  watatu Otaigo Mwema milioni 1,akifatiwa na Beatrice Mshindi wa nne na watano ikienda nafasi hiyo Kwa wote wakiambulia kiunua mgongo cha shilingi milioni 1 na zawadi za simu Kutoka Kampuni ya infinix.


Miss Tanzania Rose Manfere mwaka 2020 akimvisha taji lake Miss Tanzania 2022 mara Baada ya kutangazwa rasmi Mshindi wa kwanza akijinyakulia gari mpya aina ya Mercedes Benz class C 200 pamoja na kitita cha shilingi milioni 10 usiku wa kuamkia Leo katika ukumbi wa Mlimani city Jijini Dar es salaam.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad