Ni desturi ya Meridianbet kurejesha kwa jamii na safari hii, siku maalumu ya kusherehekea kinamama ilinogeshwa zaidi na kapu la bi mkubwa kutoka Meridianbet. Kama wanavyotambulika kwa kuwa mabingwa wa Odds na Bonasi kubwa kwenye michezo ya kubashiri, vivyo hivyo Meridianbet imewatambua na kuwaongezea tabasamu kinamama wanaojishughulisha na kazi mbalimbali za kujipatia kipato.
Wapo wasusi, wavuvi, washonaji nguo, wauza mbogamboga, wauza vyakula almaarufu ‘mama ntilie’ na wafanyabiashara wengine wengi wadogo wadogo. Wote hawa ni sehemu ndogo ya kinamama wengi nchini wanaowekeza nguvu na muda wao katika kazi ya kujipatia kipato ili kukidhi mahitaji yao na familia zao.
Kwa kutambua mchango na juhudi zao, Meridianbet ilifanya ziara fupi katika masoko ya Tandale, Manzese na Msasani jijini Dar es Salaam na kuwapongeza baadhi ya kina mama wanaofanya shughuli zao ndogo ndogo kwenye maeneo hayo.
Akizungumza na Meridianbet baada ya kupokea zawadi kutoka kwenye kampuni hiyo, mmoja ya kina mama hao (hakutaka jina lake kuwekwa hadharani), ameishukuru Meridianbet kwa kuungana nao na kuwaongezea thamani kwenye majukumu yao. Pamoja na hayo, ameiomba kampuni hiyo kuendelea kuifikia zaidi jamii na pia kuwawezesha kinamama kwa kuwaongezea kwenye mitaji yao midogo ili waweze kuzikuza biashara zao wanazozifanya.
Kwa upande wa Meridianbet, Afisa Mahusiano ya Jamii, Ndugu. Amani Maeda, amewapongeza kinamama wote nchini kwa kazi kubwa wanayoifanya hasa katika malezi ya jamii na, ameendelea kuwatia moyo kina mama wote wanaojishughulisha na kazi ndogondogo za kijikwamua kiuchumi. Bwana Maeda aliongezea kuwa, Meridianbet itaendelea kuwa karibu na jamii na itaendelea kuwafikia zaidi kwa kadiri itakavyowezekana.
Meridianbet, Nyumba Yenye Odds Bora na Bonasi Kubwa!
No comments:
Post a Comment