HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, May 5, 2022

Makampuni 37 kutoka Norway na Uingereza yachambua fursa za Uwekezaji hapa nchini

Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo Cha Uwekezaji TIC, Waziri wa Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi Mhe.  Makame Mbalawa wa (pili kulia) akiwa na Naibu katibu Mkuu (Uwekezaji) Ndg. Ally S. Gugu wa kwanza kushoto na Mkurugenzi Mtendaji wa  Naba Norway Bwana Eivind Fjeldstad katika Kikao kilichofanyika Hyatt Regency   Hotel leo tarehe 05 Mei,  2022. 

Dkt. Maduhu Kazi Mkurugenzi Mtendaji TIC akingungumza na Wawekezaji kutoka Norway  wenye makampuni makubwa wenye lengo la kuwekeza Tanzania kwenye sekta mbalimbali.



MAKAMPUNI 37 kutoka nchi ya Norway na Uk yamekutana na Wizara ya Uwekezaji, Viwanda na Biashara na Kituo Cha Uwekezaji TIC katika ukumbi wa Hyatt Regency Hotel jijini Dar es Salaam leo Tarehe 05 Mei, 2022 ili kutambua fursa mbalimbali zinazofaa kuwekezwa hapa nchini

Makampuni hayo yamepata nafasi ya kusikiliza fursa za Uwekezaji zilizopo nchini kutoka kwenye Idara na Taasisi mbalimbali zinazosimamia sekta mbalimbali zinazofaa kuwekezwa hapa nchini.

Kikao hicho kimeongozwa na Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Mhe. Makame Mbalawa (Mb) ambapo amewakaribisha wawekezaji watarajiwa kwa kuwahakikishia kuwa Tanzania ni Nchi Sahihi kwa kuwekeza kwenye sekta ya miundombinu.

Akizungumza katika mkutano huo Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Uwekezaji, Viwanda na Biashara (Uwekezaji) Ally S. Gugu amesema fursa zipo na maeneo ya kuwekeza yapo aidha mazingira ya uwekezaji yameboreshwa hivyo kuchagua Tanzania kuwekeza ni kufanya maamuzi sahihi na yenye tija kwa wawekezaji hao.

"Mazingira ya Uwekezaji ni Mazuri na yamebireshwa na huduma zote zimeimarishwa ili kumwezesha Mwekezaji kupata kile anachokitaka kwa wakati na haraka"

Mkurugenzi Mtendaji wa TIC Dkt. Maduhu Kazi amesema " TIC inajitahidi kuondoa urasimu kwa kuhakikisha kazi za wawekezaji hazipit kwa vishoka kwa kuhakikisha Kituo kinatoa huduma kwa wawekezaji wakati wote kwa kuunganisha huduma na kupunguza mlolongo wa maombi ya huduma na kuyafanya yawe ya kimtandao. TIC inahakikisha pale wanapokuwa wamekwama au wanahitaji msaada wowote wanapiga simu moja kwa moja huduma kwa wateja na TIC itaweza kuwahudumia wakati wote.

Wawekezaji hao wanapendelea kuwekeza sekta za Miundombinu, Nishati, Utalii, Kilimo, Usafurishaji, Huduma na majengo ya biashara

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad