HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, May 13, 2022

Kaya masikini kusaidiwa vibao vya anwani za makazi

 Na Amiri Kilagalila,Njombe

ILI kuhamasisha na kufikia malengo ya serikali pamoja na halmashauri katika uwekaji wa vibao kwenye nyumba kupitia zoezi la anwani ya makazi,diwani wa kata ya Uwemba halmashauri ya mji wa Njombe bwana Jactan Mtewele ameahidi kununua na kuweka vibao katika kaya masikini zote zilizopo katika kijiji cha Kilenzi.

Mtewele amebainisha hayo wakati akizungumza na wananchi wa kijiji hicho katika eneo la mradi wa maji kwa ajili ya Kilenzi uliopo katika kijiji cha Njomlole

“Nitawasaidia kaya masikini kuweka vibao na hii yote nataka tuhamasishe zoezi la uwekaji wa vibao vya anwani za makazi”Alisema Jactan Mtewele diwani wa kata ya Uwemba

Diwani wa kata ya Uwemba bwana Jactan Mtewele akizungumza na wananchi wa Kilenzi katika eneo la mradi wa maji lililopo katika kijiji cha Njomlole.
Baadhi ya wananchi wa Kilenzi wakimsikiliza diwani wao walipofika kwenye eneo la mradi wa maji.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad