HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, May 10, 2022

CHAMA CHA MUZIKI WA DANSI (CHAMUDATA)KUFANYA UCHAGUZI 11 MAI 2022

*Kwanini Luiza Nyoni, Saidi Kibiriti, Hemba na Sulus- Chamudata Mpya?*


Wanamuziki na Wadau wa Muziki wa Dansi Tanzania.
Tunapoelekea kwenye tamati ya kufanikisha CHAMUDATA MPYA kupitia Uchaguzi Mkuu wa *11 May, 2022* - niwaombe wanamuziki na wadau wote muwe WATULIVU na Kuchagua kwa MAKINI. Na pia mwelekeo wa Uchaguzi unaeleweka kupata Viongozi WAPYA kabisa kama Orodha niliyoipendekeza hapo juu inavyooonyesha.


Kazi tuliyoifanya kwa pamoja yapata miaka mitatu sasa haikua ndogo na ilikua ya kujitolea jasho na moyo wote kwelikweli.
Wengi tuliokua nao hasa wanamuziki walikata tamaa na baadhi walidharau wakidhani kwamba tusingeweza kufikia hatua hii. Baadhi ya wanamuziki hasa waandamizi tuliowaamini na kuwaheshimu ndio waliokua kikwazo namba moja cha Chamudata. Baadhi yao tuliwapa heshima na tuliwapendekeza Wapokee vijiti vya kuongoza Chama Walikataa na Walidharau hata jitihada tulizozifanya sisi ambao sio wanamuziki.
Nilichogundua Mgawanyiko wa Wanamuziki Ndio ulikua Mtaji Mkubwa Kwao kujiona kwamba Wao ni Wakubwa kutambulika mbele ya taasisi za serikali kuliko *Umoja wa kny Chama*.
Hali hiyo ndio iliyosababisha kudharaulika kwa wanamuziki pamoja na Muziki wa Dansi mbele ya Umma.


Kwa Mantiki hii ni wazi sasa tunakwenda "Kukata Mirija" yao ya ujanjaujanja na kugawanyishana kwa maslahi yao binafsi. Sauti moja inapoelekea kupatikana wote tunapaswa kufuata mkondo mmoja kurejesha heshima ya wanamuziki na muziki wa dansi kwa ujumla.


MajinaTunayoyapendekeza kupigiwa kura za *Ndiyo* tumeyafanyia uchunguzi na utafiti wa kina na kuyathitisha pasipo shaka kuweza kushirikiana nao kurejesha hadhi na heshima ya muziki wa Dansi Tanzania  na pia kukubalika mbele ya vyombo mbalimbali vya binafsi na Umma.


Bado tunayo kazi kubwa mbele yetu baada ya Uchaguzi kukijenga Chama kisimame sawasawa na kukipa Taswira Tunayoitaka Mbele ya Jamii-Kitaifa na Kimataifa, hasa baada ya *Pancha* za muda mrefu zilizosababishwa na baadhi ya viongozi wabinafsi wa nyakati zilizopita. Nguvu zetu za pamoja zisipotee *bure* kwa kutuletea viongozi wa Mihemko ambao hawajapendelezwa, wala kuthibitishwa na Wadau, Wanamuziki na wala Chombo chochote.


Hivyo, ninawaomba tuchague kwa busara kwa kuwapa kura nyingi za NDIO wagombea wetu:


1. *LUIZER MORRIS NYONI* -MWENYEKITI
2.*ABDALHA HEMBA* -M/MWENYEKITI
3. *SAIDI KIBIRITI*-KATIBU MKUU
4. *Adv. BARAKA SULUS* - N/KATIBU MKUU


Hii ndio Timu ya UONGOZI MADHUBUTI Chamudata na Kazi kubwa ya mafanikio na Maendeleo inaanzia Hapo.
Tumeshatumia Fedha na Muda mwingi kwa ajili ya kufikia Jambo hili. Tuwe Kifua mbele na Tunayo Haki ya kuhakikisha Tunawapigia Kampeni na Kura za NDIO Wagombea hawa ambao tunaamini tutavuka Nao pamoja. *Luiza Nyoni*, *Abdalha Hemba*, *Saidi Kibiriti* na *Adv. Baraka Sulus* - Viongozi Sahihi kwa ajili ya Kuongoza CHAMUDATA MPYA.


No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad