Na Humphrey Shao,Michuzi TV
Wito
umetolewa Kwa Watanzania na Kenya kuongeza mahusiano ya kitaaluma bila
kuangalia tofauti zao za Mipaka ya nchi zilizomo katika jumuiya ya
Afrika Mashariki.
Wito
huo umetolewa hivi Karibuni na Naibu Mkuu wa Tasisi ya Teknolojia ya Dar
es Salaam (DIT) ,Prof Patrick Nsimama wakati wa hafla ya kuwaaga
wanafunzi 24 waliokuja kujifunza katika Chuo hicho kupitia mradi wa
RAFIC.
Prof. Nsimama
ametaja kuwa licha ya nchi zetu kutenganishwa na Mipaka lakini Bado ni
Moja Kwa maana ya Jumuiya na Bara Zima la Afrika.
"DIT
Ndio Sehemu pekee ambayo kinajengwa kituo Cha umahiri Kwa ajili ya ICT
Kwa ukanda huu wa Afrika Mashariki hivyo ni vyema Vijana na watumishi
waliopo katika jumuiya kuja Tanzania kuchota maharifa yalipo katika
kituo hicho" Amesema Prof.Nsimama.
Aidha
Amesema licha ya kuwa tofauti ya Mipaka Bado wanafunzi wetu wameonyesha
kuwa mitaala ya ufundishwaji ayatofautiani baina ya nchi na nchi ndio
maana wanafunzi Hawa 24 kutoka Kenya wamewwza kufanya vizuri katika
mafunzo yao.
Ametaja kuwa wanafunzi hao wamewwza kujifunza Masuala ya Graphics Disigner ,Animation na Masuala ya Mtandao.
Mmoja wa Walimu kutoka Kenya walioongozana na wanafuzni kutoka Kenya akizungumza wakati wa hafla kutunukiwa vyeti wanafunzi 24 kutoka kenya
Dr.Garden Tesha akizungumza na Wanafuzni kutoka Kenya
Mratibu Radical na Mradi wa RAFIC ,Dr.Joseph Matiko akizungumz umuhimu wa mradi huo
Mmoja ya Wanafunzi kutoka Kenya akizungumza uzoefu wake katika Safari hii ya Mafunzo
No comments:
Post a Comment