Afisa
Mkuu wa wateja Binafsi na Biashara wa Benki ya NMB, Filbert Mponzi
akimkaribisha Mufti Mkuu wa Tanzania Aboubakary Bin Zubery Kwa ajili ya
kushiriki futari iliyoandaliwa na Benki ya NMB.
Mufti
Mkuu wa Tanzania Aboubakary Bin Zubery akizungumza na wateja na wadau
mbalimbali wa benki ya NMB walioshiriki katika futari hiyo.
Mufti
Mkuu wa Tanzania Aboubakary Bin Zubery na Afisa Mkuu wa wateja Binafsi
na Biashara wa Benki ya NMB, Filbert Mponzi wakiongozana Kwa ajili ya
kwenda kunipatia futari.
Kwa
kutambua thamani ya Wateja wao na umuhimu Mwezi wa Ramadhani, Benki ya
NMB imeshiriki Futari na Wateja na Wadau mbalimbali wa Dar es Salaam na
kuhudhuriwa Mufti Mkuu wa Tanzania Aboubakary Bin Zubery.
Akizungumza
wakati wa hafla fupi ya Iftari Kwa wateja wa NMB wa Mkoa wa Dar es
Salaam, Mponzi amesema NMB imeamua kufanya tukio hilo kwasababu
wanaamini kupitia mwenzi mtukufu, jamii kwa ujumla inastawishwa na Sala
zinazotolewa wakati wa mwezi huu;
“Kwa msimu huu wa Ramadhani,
Benki yetu ya NMB tunapenda kujumuhika na wapendwa wetu na wadau wengine
mbalimbali wakati wa kufuturu kwani tunaamini kupitia mwezi huu tukufu,
Jamii zetu zinastawishwa na sala za zati zinazotolewa wakati huu lakini
pia baraka kwa watu wengi na Taifa kwa ujumla”
Afisa Mkuu wa
wateja Binafsi na Biashara wa Benki ya NMB, Filbert Mponzi amewasihi
waislamu wote katika kipindi hiki cha mfungo wa mwezi Mtukufu wa
Ramadhani kutafakari juu ya maadili yatakayowaunganisha Binadamu wote,
upendo kwa familia, kufanya Toba na kuzidi kushiriki katika ibada.
Na
hii siyo mara ya kwanza kujumuika na wateja wake katika ibada ya futari
hivyo, wameamua kuendeleza utamaduni huo kwa kukutana na wadau wote wa
NMB kujumuika wakati wa Iftari.
Mponzi amemshukuru Mufti Mkuu
Sheikh Aboubakary Zubery, viongozi wote wa dini na serikali lakini pia
wateja wote na wafanyakazi wa Benki ya NMB kwa kushiriki futari hiyo.
Kwa
Upande wake Mufti Mkuu wa Tanzania Aboubakary Zubery amesema NMB
wameonyesha upendo na kujali kwa kitendo cha kuandaa futari ambayo
imewakutanisha watu mbalimbali na kujenga undugu;
“NMB
mmethamini na kujali ndiyo maana mmeona umuhimu wa kuita watu mbalimbali
kuja kufuturu futari ambayo inajenga undugu, inaweka watu karibu na
watu kufurahi, hivyo viongozi wa NMB mmetuonyesha jinsi ambavyo mmekuwa
na tabia nzuri na ya kuthamini”
Pia, Mufti Mkuu amesema wao kama
Baraza kuu la Waislamu Tanzania wamekua wadau wakubwa kwa Benki ya NMB
hivyo ametoa wito kwa Wananchi wote kufungua account za NMB kwani huduma
zao ni bora zaidi .
Monday, April 18, 2022

NMB YASHIRIKI FUTARI NA WATEJA, WADAU WAKE JIJINI DAR ES SALAAM
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment